Ruto amesema katiba inahitaji pawepo usawa katika ugavi wa raslimali na kulitaka bunge kutekeleza jukumu lake ipasavyo kwa kuhakikisha kwamba kila kaunti inapata mgao inayohitaji .
" Bunge linafaa kuhakikishja kwamba mfumo unaotumiwa kugawa raslimali unaafikia ushindi kwa wote bila kuiumiza kaunti yoyote .Inawezekana’ alisema Ruto kupitia Twitter .
Maseneta wamekosa kuafikia mfumo unaofaa kutumiwa kugawa paesa kwa serikali za kaunti . Utata huo umelemaza kupitishwa kwa mswada wa wa ugavai wa mapato .
Kabla ya mswada huo kupitishwa kuwa sheria na kusainiwa na rais Kenyatta hakuna kaunti itakayopewa fedha hizo .
Utata kuhusu mfumo unaotumiwa kwa ugavi wa pesa kw akaunti umezua mgawanyiko miongoni mwa vyama vya kisiasa huku ODM ikionekana kutofautiana na upande wa jubilee unaomwunga mkono rais kenyatta unaotaka mfumo wa sasa uliopendekezwa kutumiwa .
Mwishoni mwa wiki kiranja wa walio wengi katika senate Irungu Kang'ata's alitishia kwamba hapatakuwa na BBI endapo maseneta wa ODM hawataunga mkono mfumo huo unaopendekezwa na serikali .