Mkali wa "Lubbish" apigwa faini ya 1M kwa kuonyesha video chafu, ajitetea

abg2ifi8az7xyz9pmd5cf2a4361e9b6
abg2ifi8az7xyz9pmd5cf2a4361e9b6
Kasisi na muasisi wa kanisa la Neno Evangelism Centre Ng'ang'a sasa anahoji kuwa hakukusudia kuonyesha matiti ya mwanamke kanisani mwake.

Ng'ang'a sasa anakabiliwa na mashtaka ya kuonyesha sehemu za mama aliyekuwa anamuombea katika runinga yake ya Sasa TV.

Ng'anga anajitetea kuwa hakuwa na uwezo wa kudhibiti tukio hilo la mwanamke kuonyesha matiti yake.

Soma hadithi nyingine;

Mamlaka ya mawasiliano imemtaka kasisi huyu mwenye utata kutoa faini ya Milioni 1.

Video hii ilichapishwa katika mtandao wake wa YouTube.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa maswala ya umma Chris Wambua,

Ng'anga alipigwa faini ya Milioni moja kwa sababu za kuonyesha kipindi hicho masaa ya mchana.

Soma hadithi nyingine;

Kuna muda umetengewa kuonyesha filamu za aina hiyo katika kifungu cha sheria za Kenya.

"Hata juzi nimeshtakiwa ati nimeonyesha matiti. Sasa matiti mimi sikujua kama ilikuwa imetoka maana sio yangu."

"Sasa mimi niliwaambia mimi sijui nafanya deliverance. Nikaambiwa nitalipa milioni 1 nikakata appeal sijui kama nitapewa."

Soma hadithi nyingine;

"Wamesema nimeonyesha matiti ya mwanamke masaa ambayo sio." Ng'ang'a aliwaambia waumini kanisani.

“Sasa mimi najuwaje matiti ziko nje, na watu wa Turkana nikienda huko itakuwaje. You know the people who form the constitution hawakuita Deliverance Ministry waangalie hizo vipengele. Kama mtu akilipuka na yuko mbele ya camera." alijitetea mbele ya kanisa.