Mkasa :Watu 15 wafariki katika ajali barabara kuu ya Mombasa-Malindi

Watu 15 wameaga dunia baada ya kutokea ajali mbaya kwenye barabara ya Mombasa kwenda Malindi katika eneo liitwalo Tororo .

Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa kumi na mbili jioni siku ya jumapili na ilihusisha  Lori  lililokuwa likienda Mombasa ambalo lilibadilisha mkondo kwa ghafla na kugongana ana kwa ana  na  matatu ya abiria .

Madreva wote ni miongoni mwa walioaga dunia papo hapo  ilhali manusura watatu wapo katika hospitali ya wilaya ya kilifi wakiwa na  majeraha mabaya . Kamanda wa polisi wa pwani Rashid Yakub amesema lori hilo halikuwa na mizgo wakati wa ajali .Miili ya waliofariki imepelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya kilifi