Takriban watu 57 wameafariki katika mlipuko wa trela la kubeba mafta nchini Tanzania ,polisi wamesema . Picha zilizowekwa mtandaoni zinaonyesha moto mkubwa ukiteleteza sehemu kubwa ya eneo huku miili yenye majeraha ya moto ikitapakaa kote .
Ripoti ambazo hazina ithibati zinasema kwamba atu walikuwa wakijaribu kufyonza mafuta kutoka kwa gari hilo ambali lilibingiria wakati mlipuko ulipotokea . Kisa hicho kimefanyika Morogoro yapata kilomita 200 magharibi mwa Jiji la Dar es salaam .
Mji wa morogoro ni kitovu muhimu cha usafirishaji wa mafuta kutoka bandari ya Dar .Kuna hofu kwamba idadi ya walioangamia huenda ikaongezeka .