Mke mwema! Tazama picha za mkewe Jomo, mtoto wake Rais Uhuru

Achola na mpenzi wake Jomo ambaye ni mtoto wa kwanza wa rais Uhuru Kenyatta alifunga pingu za maisha na npenzi wake mwezi wa October mwaka wa 2016.
Wapenzi hawa wamebarikiwa na mtoto mmoja wa kike ambaye ameumbwa akaumbika.

Binti Achola, mama ya mtoto mmoja ni mwanamke mrembo sana na urembo hujakolea nje tu bali pia ndani kwani ana roho nzuri sana.

Zaidi ya hayo, binti huyu ana mtindo mufti sana wa kuvaa. Yeye huvaa nguo za heshima kana kwamba anaelewa fika kuwa wahenga hawakutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa waliposema, heshima si utumwa.
Vilevile, binti huyu huhudhuria sherehe zote ambazo mume wake huenda Aisee! Upendapo uendapo.
Tazama picha, naamini utasadiki kuwa, uzuri upo na kuwa Jomo alichagua mke mwema.