Mke wangu alinimwagilia maji moto akiwa mlevi

Kwa mara nyingi kesi za dhulma dhidi ya wanaume katika ndoa zimeangaziwa katika kipindi cha Bustani la Massawe, huku mtangazaji huyo akikashifu visa hivyo.

Rueben kutoka Kitale alipiga simu siku kadhaa zilizopita kusimulia kuwa amepitia maovu mikononi mwa mkewe mkatili.

Kulingana na jamaa huyu, mkewe ni mlevi chakari na isitoshe hawajibiki nyumbani, kwani mara nyingi yeye hufika nyumbani akiwa amechelewa au hata akiwa amelewa chakari.

Reuben anasimulia vile siku moja mkewe alimchoma na maji moto akiwa amelala, isitoshe hakuwa wawili hao hawakuwa wamekosana na mkewe alipotea baada ya kisa hicho.

Soma usimulizi wake.

Mimi nilimwagiwa maji moto na mke wangu ambaye tumeishi naye kwa miaka sita. Kisa na maana ni kuwa alikuwa analewa sana. Nilikuwa naingia kwa nyumba na yeye hajafika na nikijaribu kumwelezea hasikii kwani anakuja akiwa mlevi chakari kama amebebwa.

Siku moja nimelala kumbe ameingia kwa jiko anachemsha maji alifungua mlango na nikashtukia nimemwagiwa maji. Nilitoka pale nikiwa na kizunguzungu.

Nilipelekwa na wazazi wangu hospitalini ambapo nililala hospitalini miezi miwili kabla ya kupata nafuu.

Kitu kilichoniuma sana ni kuwa alienda kwao na sikumfanyia chochote, niliwaita wazazi wake wamchukua na mpaka sahii nikasema mungu pekee ndio anajua na nikawachana naye.