Mke wangu alitaka kunidunga na kisu alipogunuda nina mpango wa kando

Obadiah alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe ambaye wameoana kwa miaka minane. Alidai mkewe Grace walikosania swala la mpango wa kando.

"Ilikuwa kitu June tarehe 11 wakati mke wangu aligundua nina mpango wa kando. Huyo msichana alikuwa rafiki wa Grace wa ndani kabisa na pia akawa rafiki wa familia. Tulikuwa tunashinda naye na akaja akajua siri za familia yetu zote na tukikosana na bibi kidogo anajua.

Sasa akachukua hiyo nafasi tukaingiana naye, kitu kama mwezi wa nne mimi naye tukawa karibu kabisa na kufikia June tukaanza urafiki.

Bibi alijua na akaondoka mara ya kwanza lakini tukazungumza na akarudi, Jumapili moja bibi alianza kurudi kwenda kumuuliza shida ni gani akaanza kulia na kudai kuwa nilikuwa nimetoka kwa Reginah." Alieleza Obadiah.

&feature=youtu.be