Mkenya mwingine afariki kutokana na COVID-19 ng'ambo

unnamed (3)
unnamed (3)

Mgonjwa wa pili, ambaye ni Mkenya ameaga dunia kutokana na ugonjwa wa Coronavirus huko Massachusetts , nchini Marekani.

Familia yake inasema alikuwa akipokea matibabu ya ugonjwa tofauti aliokuwa akiuguza alipofariki kutokana na virusi hivyo Jumatano juma lililopita.

Mwili wake utateketezwa jumatano wiki ijayo.

Hayo yakijiri mamlaka ya kutathmini utendakazi wa polisi IPOA itaanzisha uchunguzi wa madai ya matumizi ya nguvu kupita kiasi katika kuhakikisha watu wanazingatia marufuku iliyowekwa na serikali ya kutotoka nje kati ya saa moja usiku na saa kumi na moja asubuhi.

Mwenyekiti Anne Makori anasema polisi hao wanastahili kufuata sheria hata wanapotekeleza maagizo ya serikali.

Kwingineko, wakaazi wa Nairobi wanaoishi katika mitaa ya mabanda  watapokea maji bila malipo.

Mkurugenzi mkuu wa jiji Jenerali Mohammed Badi anasema hii itaisaidia serikali kwa juhudi zake za kukabiliana na maambukizi ya Coronavirus.