Mkono wa mhisani! Evans Oluoch asambaza barakoa Kibra

EYCxmWPXQAAYPKu
EYCxmWPXQAAYPKu
Evans Oluoch ambaye ni nduguye Ken Okoth ambaye alikuwa mbunge wa Kibra, ameamua kuwasambazia wakaazi wa mtaa wa Soweto eneo hilo barakoa na vitakasa mikono kama njia ya kuwasaidia wakaazi hao kudumisha usafi wakati huu ambapo virusi hivyo vinaendelea kupenya katika vitongoji mbalimbali nchini.

Mtaa wa Kibra umeanza kuipa serikali changamoto hasa baada ya jamaa mmoja aliyefariki katika kaunti ya Bomet kubainika kuwa alikuwa anaishi mtaa huo.

Visa kadhaa vimekuwa vikiripotiwa kutoka Kibra hatua ambayo imewafanya baadhi ya wahisani kujitokeza na kuwapa wakaazi ufadhili wa barakoa.