Mkufunzi Sarri alitusaliti: Napoli yalia kuhusu Juventus

Mshambulizi wa Napoli Lorenzo Insigne amesema kuwa aliyekuwa mkufunzi wa timu hiyo maurizio sarri alisaliti klabu ya Napoli kwa kukubali kujiunga na klabu ya Juventus.

Sarri alikuwa mkufunzi wa Napoli kwa misimu mitatu huku katika misimu yote akimaliza katika nafasi ya pili huku Juventus ikitwaa taji nyakati hizo zote.

Kwa sasa, Sarri ndiye mkufunzi mpya wa Juventus baada ya kutia sahihi kandarasi ya miaka mitatu. Insigne kwa sasa ndiye nahodha wa Napoli. Alitia mkataba wa miaka minne msimu uliopita huku akisema kuwa matamanio yake ni kustaafu soka akikipigia Napoli.

Klabu ya Liverpool inatarajiwa kuwasilisha ombi la kumchukua tena aliyekuwa kiungo mshambulizi wao Phillipe Coutinho. Baada ya ujio wake Griezmann, Coutinho amejipata katika hali tatanishi na inakisiwa kwamba anataka kuondoa ugani Camp Nou ilikurudisha makali yake.

Everton imemsajili kiungo wa Manchester City, Fabian Delph kwa mkataba wa miaka mitatu. Delph mwenye umri wamiaka 29 amejiunga na klabu hio kwa dau la millioni 9. Akivalia jezi ya Manchester City, Delph alishida kombe la ligi kuu nchini uingereza mara mbili.

Neymar amewaeleza kinagaubaga mabosi wake wa PSG kuwa yupo tayari kuhama klabu hio. Neymar alikutana na wadosi wake hio jana kwenye mkutano wa siri na ilifichuka kuwa neymar yupo tayari kuihama PSG.