Wazazi wameshauriwa kukoma kuwapa shinikizo wanafunzi kufanya vyema katika mitihani ya kitaifa .waziri wa elimu George Magoha pia amewataka watahiniwa wa mwaka huu kutoitikia kuwekwa chini ya shinikizo kwani kila mmoja atasonga katika hatua ifuatayo ya elimu bila kujali matokeo yake .
TSC imewapiga marufukua walimu waliohusika na visa vya udanganyifu katika mitihani ya hapo awali dhidi ya kusimamia mitihani ijayo ya KCPE na KCSE . Afisa mkuu wa tume hiyo Nancy Macharia amesema katika miaka mitatu iliyopita ,wamewachukulia hatua walimu 144 waliohusika na udanganyifu katika mitihani ya kitaifa .
Kiongozi wa walio wengi katika bunge la kaunti ya Nairobi Abdi Guyo ameandikisha taarifa na DCI akidai kamba maisha yake yamo hatarini . Amesema kizazaa kilichotokea city hall wiki jana kilipangwa na magenge yalitumwa katika bunge la kaunti kusambaratisha shughuli .
Mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za marathon Eliud Kipchoge ametaka kukutana na rais wa zamani wa marekani Barrack Obama .hii ni baada ya Obama kumtumia ujumbe wa kumhongera katika twitter kwa kumudu kumaliza mbio za marathon chini ya saa mbili .Obama pia alimtambua Brigid Kosgei kwa kuvunja rekodi ya akina dada katika mbio za marathon..Kipchoge anataka kukutana na Obama ili kujadili jinsi ya kuufanya ulimwengu kuwa bora zaidi .
Wakaazi wa Mombasa wanaitaka serikali kuboresha usalama katika feri ili kuzuia maafa siku za usoni . wamesema baadhi ya sehemu za feri zinafaa kuboreshwa na pia kuweka vifaa vya kuwawezesha watu kujiokoa wakati panapotokea dharura .