Mahakama ya leba leo imeamuru kwamba Wilson Sossion anaweza kushikilia nyadhifa mbili ,kama katibu mkuu wa muungano wa walimu Knut na kama mbunge maalum . jaji Maureen Onyango ameamuru kwamba hakuna kinachokiuka katiba kwa session kushikilia nyadhfa hizo mbili .wanaopinga Sossion kufanya kazi zote mbili walitaka aondolewe KNUT kwa sababu ya kazi yake kama mbunge
Muungano wa wauguzi umeukataa mswada wa punguza mizigo ukisema haushughulikii mahitaji ya wauguzi .katibu mkuu Sethn Panyako amesema kiongozi wa Tirdway Alliance anautumia mswada huo kuendeleza ajenda zake kisiasa .
Afisa mkuu mtendaji wa IPOA aliyefutwa kazi Maina Njoroge amerejeshwa kazini . mwenyekiti wa maamlaka hiyo Anne Makori amesema mkuu wa sheria alitilia doa uamuzi wa kumfuta kazi Maina aliyetofautiana na bodi ya maamlaka hiyo.
Rais Uhuru Kenyatta ametoa msaada wa shilingi milioni 2 kwa wazazi wa shule ya precious talent baada ya mkasa uliosababisha vifo vya wanafunzi wanane . kiongozi wa ODM Raila odinga naye ametoa shilingi milioni 1 akisema silingi milioni moja ni za kuwafariji wazazi walioafiwa ilhali milioni 2 ni za kujenga shule .
Mahakama kuu imeamuru kwamba picha ya Mzee jomo Kenyatta iliyotumiwa katika noti mpya sio ukiukaji wa katiba kwani pucha hiyo ni sehemu ya jumba la KICC . majaji kanyi kimondo na Asenath Ongeri wamesema CBK haikukika sheria kwa kutumia picha hiyo katika sarafu mpya .
Serikali imeifunga shule ya msingi ya Green field huko changamwe kwa sababu majengo yake sio salama . waziri wa elimu George Magoha pia ameagiza shule iliyo karibu ya Umoja kuwachukua wanafunzi 445 waliokuwa wakisomea katika shule ya Greenfiled .
Watu 15 wameorodheshwa kuwa miongoni mwa wanaozingatiwa kwa nafasi iliyo wazi ya mratibu mkuu wa bajeti .mionngoni mwao ni wanawake sita ili kuichukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Agnes Odhiambo ambaye hatamu yake ilitamatika mwishoni mwa mwaka huu mahojiano yataanza tarehe 9 mwezi ujao .
Maafisa wote 75,000 wa polisi watakuwa na sare mpya za samawati kufikia mwaka wa 2021 .katibu wa kudumu wa usalama wa ndani karanja Kibicho amesema sare elfu 16 tayari zimetengezwa huku nyingine elfu 20 zikitarajiwa kuwa tayari kufikia mwisho w amwaka huu wa kifedha .
Mmiliki wa shule ya Precious Talent Moses Ndirangu atasalia rumande kwa siku 15 ili kuwaruhusu polisi kukamilisha uchunguzi . mahakama ya kibera pia imewaagiza polisi kupata ripoti kutoka wizara ya elimu na idara ya mipango ya jiji ili kuwasaidia katika uchunguzi wao .
Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 7 wa gredi ya pili ametoa hotuba yenye hisia za simaniz kuwakumbuka wenzake walioaga dunia baada ya kuporomoka kwa jengo la madarasa ya shule ya msingi ya precipus talent . wengi waliohudhuria misa ya wafu ya wanafunzi wanane walioaga dunia katika mkasa huo walishindwa kujizuia kububujikwa machozi wakati Abilash Muthoni alipokuwa akitoa hotuba yake .