Polisi huko Gilgil wamemkamata mwanamme mmoja aliyemlaghai mwakamke shilingi elfu 720 kwa ahadi ya kumsaidia kuwaingiza wanawe wawili katika jeshi . Mshukiwa aliyejifanywa kuwa kapteini katika KDF alikamatwa katika chumba cha hoteli moja akingoja kupokea pesa zaidi . Polisi walifaulu kunasa barua feki za usajili kutoka kwa mshukiwa huyo huku wakigundua kwamba huenda waathiriwa zaidi walipunjwa fedha na mshukiwa huyo .
Mtu mmoja afariki kwa kugongwa na Treni Changamwe
Mwanamme mmoja ameaga dunia baada ya kugongwa na treni ya kubeba mizigo katika eneo la bikirani huko changamwe . mwathiriwa alikuwa akivuka njia ya reli wakati alipogongwa mapema leo .wakaazi sasa wanalitaka shirika la reli kujenda kivukio cha kuviunganisha vijiji vya kwa punda na Bikirani .
James Mburu ateuliwa kuwa kamishna mkuu mpya wa KRA .
Waziri wa fedha Henry Rotich ametangaza uteuzi wa james mburu kama kamishna mkuu wa halmashauri ya KRA . Mburu atahudumu kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia julai mois mwaka huu .kwa sasa anahudumu kama kamishna wa KRA kuhusu uchunguzi na oparesheni maalum
Juhudi za kuwaokoa Waliozikwa na udongo wa shimo la choo Nyeri zaendelea .
Shughuli ya kuwatafuta watu watatu waliozikwa hao katika shimo la choo huko nyeri inaendelea . kamanda wa polisi Adiel Nyange amesema shughuli hiyo imeanza saa mbili asubuhi leo na wana matumaini ya kuwapata hai licha ya juhudi za kuwaokoa kuchukua saa 24 .
Sonko afutilia mbali kandarasi ya ununuzi wa magari ya City Hall
Gavana wa Mike Sonko amefutilia mbali kandarasi ya shilingi milioni 400 ya ununuzi wa magari ya maafisa wakuu wa City hall .sonko amesema fedha hizo zitatumiwa kununua magari ya ambulansi na ujenzi wa barabara .
Filamu ya Rafiki itachezwa Kortini kama ushahidi
Filamu yenye utata kwa jina rafiki itachezwa kortini kama ushahidi katika kesi iliyowasilishwa na mwelekezi wake wanuri kahiu . Korti imesema kuicheza filamu hiyo mahakama haitachelewesha kusikizwa kwa kesi hiyo kama lilivyodai shirika la filamu nchini .