Mkusanyiko wa Habari na Matukio Muhimu Ijumaa 7 Juni 2019

 Hakuna kugawana mali nusu kwa nusu wakati ndoa inapoisha .

 Mahakama moja ya Muranga  imeamuru kwamba  mwanandoa  hafai kupata nusu ya mali  moja kwa moja  wakati wanapotalakiana . Jaji Kanyi Kimondo amesema  kugawana mali kunafaa kutegemea mchango wa kila mwanandoa  .Amesema pia kila mtu anafaa kuwa na ushahidi wa kuthibitisha mchango wake katika mali hiyo kabla ya kuiitisha kutoka kwa mwenzake .

  Waaandamajai wakatiza usafiri mlolongo katika barabara kuu ya Nairobi –Mombasa

Usafiri  umekatizwa leo  katika  barabara kuu ya  Nairobi kwenda Mombasa  huko mlolongo wakati  waandamanaji  walipoiziba  kulalamikia  ongezeko la visa vya uhalifu . Polisi  wamekabiliana na waandamanaji hao kwa kuwarushia vitoa machozi na wamewashauri wenye magari kutumia njia mbadala .

  Uvutaji ya shisha ni hatari kuliko hata sigara

Uvutaji wa shisha unaweza kudhuru  mapafu yako haraka kuliko hata uvutaji wa sigara .Joel Gitali kutoka  tobaco Alliance  amesema vijana wengi wamekuwa wakivuta shisha wakifiri madhara yake  sio mabaya kama  sigara .

 Acheni uhalifu ,Sonko awaonya vijana

Gavana wa Nairobi  Mike Sonko  amewahimiza vijana wanaojihusisha na uhalifu kukoma wovu huo na kuchukua hatua za kubadilisha mtindo wa maisha yao .Sonko amesema yuko tayari kuwasaidia vijana hao  kujirekebisha ili kuepuka kuuwa na polisi .

  Bilioni 7 kutumia kuzuia mafuriko Budalang’o na Siaya – Ruto

Serikali itatumia shilingi bilioni 7  kujenga mitaro na kuweka vizuizi vya kukabiliana na mafurko  huko Budalangi na Siaya .Naibu wa Rais William Ruto  amesema ukuta thabiti na mrefu utajengwa   katika maeneo hayo  ili kuthibiti maji ya mvua .

  Wanakandarasi wataka kulipwa na Gavana Waiguru

 Zaidi ya wanakandarasi 100 huko kirinyaga wamempa gavana Anne Waiguru  makataa ya siku 30 kuwalipa deni lao la shilingi zaidi ya milioni 400 . Fedha hizo ni malimbikizi ya pesa  za huduma na bidhaa walizoipa kaunti hiyo tangu mwaka wa kifedha wa 2015-2916 .

  Hakuna maji Mombasa na Kilifi

 WAKAAZI  wa Mombasa  na kilifi watakosa huduma za maji  baada ya umeme katika kituo  kikuu cha maji kukatizwa kwa ajili ya kutolipwa kwa bili . kampuni ya maji ya mombasa  imetoa ilani hiyo kwa wakaazi baada ya wasambazi wa maji katika maeneo ya malindi na kilifi kukosa kulipa shilingi milioni 2 .

  Polisi wanafaa kuongeza mishahara –Babi Owino

Mbunge wa Embakasi mashariki  Babu Owino  amependekeza mswada  unaolenga kuwaongeza polisi mishahara .Mswada huo  unalenga kuishurutisha tume ya kitaifa ya polisi kuwalipa polisi kulingana na  kazi  wanayofanya

    Tutatekeleza vyema kazi ya kuunda sare za polisi –NYS

 Shirika la NYS  limeapa  kutekeleza ahadi yake ya kutengeza sare mpya za polisi .Kaimu  mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Matilda Sakwa  amesema kufikia mwisho wa mwezi huu ,sare  zaidi ya elfu 16 za polisi zitakuwa tayari

 Hakuna kupunguza umri wa mtu kufanya mapenzi –Matiang’i

Pendekezo  la kupunguza umri  wa  mtu kufanya mapenzi  kama mtu mzima  halitakubalika .waziri wa usalama wa ndani Fred matiangi  amesema hatua hiyo itahatarisha maisha  ya vijana wadogo

 Wizara ya leba na KNBS kufanya utafiti wa sekta ya juakali

Wzara  ya leba  na  shirika la takwimu nchini  zitafanya utafiti wa kitaifa  ili kuratibu ujuzi na uwezo wa sekta ya jua kali .Waziri wa leba Ukur Yattani  amesema shughuli hiyo ya siku 40 itakayoanza jumatatu inalenga kutambua  mahitaji ya uajiri na ukuaji wa taaluma katika sekta hiyo .