Mkusanyiko wa Habari na Matukio Muhimu Jumatatu 8/10/2019

RADIO JAMBO MIC
RADIO JAMBO MIC
 Hazina ya NHIF imetoa tahadhari kwa wananchi kuwa wangalifu kuhusu  walaghai wanaojifanya kuweza kuwapa huduma zilizoboresha chini ya bima hiyo . NHIF imesema  yeyote anayelenga  kufanya boashara nayo anafaa kuzuru afisi zake , vituo vya huduma au kupitia tovuti yao.

Kitambulisho kilichopotea kilitumiwa kuisajili kadi ya simu iliyotumika katika mauaji ya wakili wa IPOA Willie kimani na watu wengine wawili . Moses kariithi ambaye  kitambulisho chake kilitumika kuisajili  laini ya simu iliyotumika amefika kortini leo kueleza kwamba kitambulisho chake kilipotea mwaka wa 2016 . aliripoti  kupotea kwa kitambulisho hicho katika kituo cha polisi cha mlolongo na kisha akpewa kingine katika kituo cha Huduma .

Via vya ghasia  na vya watu kujiua  au matukio ya kutamaushwa ni mazngira mabyo huenda  yakachangia  mtoto kujaribu kujiua . mwanasaikolojia Riziki Ahmed  amesema watoto kupitia nykati ngumu na ni muhimu kwa  wazazi kuunda uhusiano  wa kuwawezesha kustahimili changamoto hizo .

Mahakama ya juu zaidi imetupilia mbali  pingamizi ya bunge  kuhusu maamlaka yake ya kutoa maoni ya ushauri  katika kesi iliyowasilishwa na serikali za kaunti kuhusu ugavi wa mapato . korti  hiyo imesema maelekezo kuhusu masuala yote yalioibuliwa yatatolewa  jumatano wiki ijayo.

Bunge la kaunti ya nakuru limeukataa mswada wa punguza Mizigo  ,na kufikisha tano kaunti ambazo zimeukataa mswada huo   kufikia sasa .spika Joel Maina  amesema miongoni mwa sababu za kuukataa mswada huo ni pendekezo la kuvunjilia mbali maeneo bunge hatua anayosema itavuuga ugatuzi .

Vijana wanajiingiza katika utumizi wa dawa za kulevya wakiwa na umri wa miaka 13 .ufichuzi huo umo katika ripoti iliyotolewa na shirika la nacada  kwa wizara ya elimu  inayoeleza utumizi wa mihadarai miongoni mwa watoto wa shule .

Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala za rambi kwa familia ,jamaa na rafiki za mwanafalsafa na msomi Samuel Mbiti . Uhuru amemtaja Mbiti  kama msomi mashuhuri  ambaye amekuwa kielelezo kwa wakenya wengi na alikuwa balozi muhimu sana wa Kenya   katika mataifa ya nje .

Kamati ya senate kuhusu uhasibu imezidisha  muda wa waranti ya kukamatwa kwa gavana wa machakos Alfred Mutua  kwa wiki mbili baada ya gavana huyo kukosa kuwasili mbele ya kamati hiyo kwa mara ya pili leo . mwenyekiti wa kamati hiyo moses kajwang  amesema hatua hiyo ya mutual ni kukaidi maamlaka ya bunge na pia ni ukiukaji wa sheria .