SERIkali itatumia shilingi bilioni 326 kwa idara za usalama mwaka huu wa kifedha .waziri wa fedha Henry Rotich amesema usalama wa kitaifa ni nguzo muhimu sana katika kuhakikisha uthabiti wa kiuchumi na kuwavutia wawekezaji
Kwingineko serikali imeitengea tume ya kupamabana na ufisadi shilingi biloni 2.9 na shilingi bilioni 3 kwa afisi ya DPP ili kupiga jeki vita dhidi ya rushwa .waziri wa fedha Henry Rotich amesema shilingi bilioni 5.7 zitakabidhiwa afisi ya mkaguzi mkuu wa mahesabu ya Umma .
Hospitali ya kitaifa ya Kenyatta imetngewa shilingi bilioni 14.4 ili kuboresha huduma zake kwa wananchi ..waziri Henry Rotich pia ameitengea hospitali ya rufaa ya Moi shilingi bilioni 9.2 .
Ajenda kuu nne za rais uhuu Kenyatta zimetengewa shilingi bilioni 450 katika bajeti ya mwkaa wa kifedha wa 2019/20 .waziri wa fedha Hnery Rotich amesema mgao huo ni pamoja na shilingi bilioni 47.8 za mpango wa afya ya gharama ya chini UHC ambao pia umepata shilingi bilioni 7.9 kutoka hazina ya spoti na sanaa
Kampuni za michezo ya bahati nasibu zimepata pigo baada ya kuongezwa kodi nyingine ya asilimia 10.waziri wa fedha henry Rotich amesema hatua hiyo imechukuliwa kuwazuia vijana kushiriki michezo ya bahati nasibu .
NTSA yazipokonya leseni shule 51 za Udereva
Maamlaka ya NTSA imefutilia mbali leseni za kuhudumu za shule 51 za udereva ambazo zilikosa kuwasilisha stakabadhi za kupewa leseni mpya .shule hizo zipo katika kaunti 16 na hazitaweza kupata huduma za NTSA mtandaoni .
Wachina 7 waliokuwa wakiuza mitumba Gikomba warejeshwa nchini mwao
Raia saba wa Uchina waliokuwa wamefungua biashara ya kuuza nguo za mitumba katika soko la Gikomba wamerejeshwa nchini mwao .wizara ya usalama wa ndani imesema watatu kati yao hawakuwa na vibali halali ya kufanya kazi nchini ilhali wanne walijihusisha na biashara na shughuli za kujipa mapato kinyume na matakwa ya vibali vyao.
Jane Mariott ndiye balozi ajaye wa Uingereza nchini Kenya
Mtaalam wa kupambana na ugaidi Jane Mariott ndiye balozi ajaye wa Uingereza humu nchini kuanzia septemba mwaka huu . ataichukua nafasi ya Nic Hailey ambaye amekuwa nchini tangu mwaka wa 2015 .
wabunge na maseneta wakosa kuafikiana kuhusu mgao wa fedha za bajeti kwa kaunti
Kamati ya upatanisho kuhusu mswada wa ugavi wa mapato imekosa kukubaliana muda mfupi kabla ya waziri wa fedha Henry Rotich kuisoma bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2019/2020 . utata umesababishwa na hatua ya maseneta kutaka kaunti zipewe shilingi bilioni 327 huku wabunge wakisema shilingi bilioni 316 zitazitosha kaunti .
Wakaazi wa kisauni wapata kituo kipya cha polisi
Wakaazi wa kisauni wametakiwa kukitumia kituo kipya cha polisi kilichofunguliwa katika eneo hilo ili kukabiliana na visa vya uhalifu .kamishna wa kaunti hiyo Evans Achoki amewataka wakaazi kushirikiana na polisi kwa kuripoti visa vya uhalifu .
Mtego wa Bomu la al shabaab wawauwa washukiwa 3 wa kundi hilo Boni
Bomu la kujitengezea ambalo washukiwa al shabaab walikuwa wakilitega kando ya barabara katika msitu wa Boni imelipuka na kuwauwa washukiwa watatu wa kundi hilo .polisi wanasema bunduki tatu za AK 47 ni baadhi ya silaha zilizopatikana katika eneo la tukio .
Mbunge amshambulia mwenzake bungeni
Mbunge wa wajir mashariki Rashid Amin ameshtumiwa kwa kumshambulia mwakilishi wa akina mama wa wajir FATUMA Gedi katika majengo ya bunge mapema alhamisi . kisa hicho kilifanyika katika eneo la kuegesha magari bungeni wakati Bi.Gedi alipokuwa na mwakilishi wa akina mama wa homabay Gladys Wanga .
Mbona wanwake hawaripoti dhlma za kijinsia ?
Woga ,fedheha ,ufisadi na utepetevu wa polisi ndio baadhi ya sababu ambazo huwafanya wanawake kukosa kuripoti dhulma za jinsia . utafiti uliofanywa katika mitaa ya mabanda hapa Nairobi umeonyesha kwamba waathiriwa wengi waliwashtumu polisi na maafisa wa utawala kwa kupokea rushwa kutoka kwa washukiwa wa dhulma hizo
Mwathiriwa wa pili wa ebola aaga dunia Uganda
Mwanamke mmoja raia wa Congo ndiye mgonjwa wa pili kuaga dunia nchini Uganda akwa ajili ya ugonjwa wa ebola . mwathiriwa huyo ni nyanyake mtoto wa miaka mitano aliyeaga dunia hapo jana baada ya kuvuka mpaka na kuingia Uganda kutoka DRC siku ya jumanne .
Barabara zinazopakana na bunge kufungwa kwa ajili ya kusomwa kwa bajeti
Tume ya uchaguzi na mipaka imeyaratibu majina ya watu kumi wanaozangatiwa kwa nafasi ya afisa mkuu mtendaji ili kuichukua nafasi iliyoachwa wazi na Ezra Chiloba . watatu kati yao ni wanawake .tume hiyo imesema ilipokea maombi kutoka kwa watu 90 .
Afisi ta DPP itawalinda mashahidi wote
Afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma imetoa hakikisho kwamba itawalinda mashahidi wote bila kujali kesi ambazo mashahidi hao wanatumiwa kutoa ushahidi wao . Naibu mkurugenzi Edwin Okello amesema kila mtu anayeripoti uhalifu ana haki ya kulindwa na idara hiyo .