Mkusanyiko wa Habari na Matukio Muhimu Tarehe 18 Juni 2018

 Vijana kupewa mikopo kwa riba ya asilimia 9 

Rais Uhuru Kenyatta amefaulu kuafikia makubaliano na benki kuhusu mbinu bora za kuwapa vijana mikopo nafuu, almaarufu Stawi. Baada  ya  mashauriano na Rais, benki sasa zitaanza kutoa mikopo kwa riba ya asilimia 9 kwa vijana ili kuwasaidia kuanzisha shughuli za kujipa mapato.

Hazuna ya kitaifa kutoa pesa inazodaiwa kufikia mwisho wa mwezi 

Hazina ya kitaifa  itatoa shilingi bilioni 65  inazodaiwa kufikia mwisho wa mwezi huu .  hilo limetangazwa leo wakati wa mkutano kati ya magavana na naibu wa rais william Ruto .

  Maafisa wa usalama hawafai kuuawa hivi-mtaalam wa usalama 

Udhaifu  wa kufanya mipango na mikakati ya kiusalama ndio hatua inayofaa kulaumiwa kwa mauaji ya maafisa wa polisi .mtaalam wa masuala ya usalama Byron Adera  amesema matumizi yafaayo na habari za ujasusi na  mwongozo mzuri wa maafisa wa usalama ni  mambo yanayofaa kuboreshwa ili kuzuia mauaji ya polisi katika jitihada za kukabiliana na ugaidi .

    Rais Uhuru  Kenyatta kuwateua Makamishna wa NCIC

Makamishna wa tume ya kitaifa ya Uwiano na utangamano  sasa watateuliwa na rais  na kuidhinishwa na bunge . marekebisho ya sheria sasa yanawaondoa  wenyeviti wa  tume  ya haki za binadamu ,tume ya jinsia na usawa na ile ya usimamizi wa haki  kuhusishwa katika uteuzi huo .

  IMLU yataka uchunguzi zaidi kuhusu kifo cha mfungwa Naivasha 

 Shirika la Independent medical LEGAL Unit linataka uchunguzi wa kina kufanywa ili kubaini kilicho sababisha kifo cha mfungwa mmoja katika gereza kuu la naivasha . Samuel gitahi anadaiwa kupigwa na maafisa wa gereza hilo  tarehe 13 mwezi huu baadaye akaaga dunia .

Sakwa ateuliwa rasmi kuwa mkuu wa NYS 

Matilda Sakwa  amethibitishwa kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la NYS . Sakwa ameteuliwa na rais uhuru kenyatta kupitia arifa ya gazeti rasmi la serikali   ya tarehe 30 mei mwaka huu .

 Wasioweza kuona walalamikia muundo wa noti mpya 

 Watu wenye ulemavu wa kuona   wamelalakimia muundo wa noti mpya zilizotolewa na benki kuu kwani hazina  alama za kutosha kuwawezesha kuzitambua . wamesema itakuwa vigumu kwao kuzitofautisha noti hizo  .

  Mtalii aliyekamatwa kwa ubakaji aachiliwa huru 

  Mtalii mmoja wa raia wa ujerumani aliyeshtumiwa kwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka minane  ameachiliwa na mahakama   moja ya malindi  baada ya kupatikana kwamba hana hatia . korti imesema kwamba  upande wa mashtaka ulikosa kuthibitisha kwamba Karl Ottomon alitekeleza kosa hilo

Jowie anyimwa dhamana kwa mara ya pili 

Mahakama kuu kwa mara ya pili imemnyima  dhamana mshukiwa wa mauaji Joseph Irungu kwa jina jingine Jowie . Korti imekataa ombi la Jowie ikisema halina msingi wowote .

     Utalipia huduma za visa kutumia noti za kale 

 Wakenya wanaolenga kusafiri kwenda marekani wameshauriwa kulipia visa zao au huduma zozote katika ubalozi wa amerika kutumia noti za kale .ubalozi wa amerika nchini umesema unatayarisha  utaratibu wa kuzikubali noti mpya zilizozinduliw ana serikali mwanzoni mwa mwezi huu .

 Mawingu ba baridi ndio hali itakayoshuhudiwa katika sehemu nyingi 

 Hali ya mawingu itashuhudiwa katika nyanda za juu za kati ikiwemo Nairobi  katika siku tano zijazo  . idara ya utabiri wa hali ya anga  imesema mvua zitashuhudiwa katika maeneo ya  ziwa victoria , magharibi ,kati na kusini mwa Rift valley . upepo mkali pia unatarajiwa katika nusu ya mashariki ya taifa  na katika ukanda wa pwani .

Wahadhiri wa chuo cha matibabu cha Moi wagoma 

Wahadhiri   katika chuo cha mafunzo ya matibabu cha Moi  wamegoma  wakitaka kulipwa malimbikizi ya marupurupu  ya huduma za kliniki . katibau mkuu wa  muungano wao  ISHAMEL  Ayabei  amesema usimamizi wa chuo kikuu umeshindwa  kuonyesha kujitolea   kulipa fedha hizo  tangia  januari mwaka wa 2017 . Wameapa kulemaza shughuli zote za masomo hadi  walipwe marupurupu hayo .