Mkusanyiko wa Habari na Matukio Muhimu Tarehe 23 Juni 2019

Kaunti ya Nairobu kuwaajiri vibarua na Wanaojitolea kufanya kazi bila malipo-Sonko

Kaunti ya Nairobi sasa itawazingatia  wanaojtolea kufanya kazi bure na vibarua wakati inapowaajiri wafanyikazi wake .Gavana Mike Sonko amesema  ameagiza bodi ya kuwajiri wafanyikazi ya kaunti kuhakikisha kwamba watu ambao wamefanya kazi kama vibarua au kwa kujitolea kwa muda mrefu wanapewa ajira endapo pana fursa .

 Uasin Gishu yapokea miche Elfu 10 ya Parachichi kutoka kwa Murang'a

Kaunti ya Uasin Gishu  Imepokea  miche  elfu kumi ya   avocado  kutoka kwa serikali ya  kaunti ya Muranga ili kusambazwa kwa wakulima . Afisa   mkuu wa kilimo cha biashara  wa Murang’a Bernard Kariuki  amesema hatua hiyo imetokana na ahadi aliotoa gavana  wa Murang’a Mwangi Wa Iria alipozuru  Uasin Gishu mapema mwaka huu .

Mabalozi wa Mashariki ya Kati waahidi kuwasadia wakaazi wa mitaa ya mabanda  

Mabalozi kutoka  mataifa ya mashariki ya kati wameahidi  kuboresha hali ya maisha ya wakaazi wa mitaa ya mabanda katika eneo la saboti . Mabalozi hao wa saudi arabia, kuwat na  UAE  wamesema wataunda ushirikiano  kati ya mataifa yao na serikali ya Kenya ili kuyapa msaada makundi ya waliotengwa

 Suluhisheni uatata wa ugavi wa fedha za kaunti-Oparanya

Baraza la magavana linawataka maseneta na wabunge kusitisha mzozo  kuhusu ugavi wa  pesa kwa serikali za kaunti .Mwenyekiti Wycliffe Oparanya ambaye pia ni gavana wa kakamega amesema serikali za kaunti  zimepata changamoto  kuidhinisha bajeti  yazo bila  kufahamua kiasi cha fedha zilizotolewa kwa kila kaunti .

Mgomo wa Madaktari Kisumu unaingia siku ya 3 

Huduma za matibabu  zimeendelea kuathiriwa huko Kisumu   kwa ajili ya mgomo wa madaktari unaoingia siku ya tatu . Madaktari ambao wameapa kutorejea kazini hadi makubaliano yao ya CBA ya mwaka wa 2017 yatekelzwe wamewashauri wakaazi kutafuta matibabu katika hospitali za kibinafsi .

  Taita Taveta inahitaji walmu zaidi wa chekechea 

Kaunti ya Taita Taveta ingali inakabiliwa na   uhaba wa walimu wa chekechea, hali ambayo inawalazimu wazazi kugharamika zaidi kulipa walimu wa ziada , kwani walioajiriwa na serikali hawatoshi.Afisaa mkuu wa elimu  wa kaunti hiyo Philomena Kirote amekiri kuwa bado  hawajaweza kuafikia idadi ya walimu ambao watahudumia watoto walio katika shule za chekechea.

Kesi ya mauaji dhidi ya Jowie na Maribe kuanza jumanne 

Kesi ya mauaji ya mfanyibiashara Monica Kimani itaanza jumanne . upande wa mashtaka umewatayarisha mashahidi 33 kutoa ushahidi dhii ya  mwanahabari Jackie Maribe na Joseph Irungu .Monica aliuawa katika nyumba yake  mtaani kilimani septemba mwaka jana .

 Utaendelea kutuma maombi ya paspoti mpya baada ya Agosti 31

  Unaweza kutuma maombi ya kupewa paspoti ya kisasa ya elktroniki hata baada ya muda wa makataa wa agosti tarehe 31 .Idara ya uhamiaji imesema  muda huo wa makataa ulikuwa wa kutumiwa kwa paspoti za kale na sio kwa mamombi ya paspoti mpya .

Acheni kuwanyanyasa wakenya kutumia mwafaka wa Kenyatta na Odinga -Mudavadi

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi ameonya kuwa wakenya hawatavumilia makosa ya serikali kwa sababu ya kuwepo kwa maafikiano baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa upinzani Raila Odinga. Mudavadi  amesema kwamba kila mkenya ana haki kuchangia katika kuundwa kwa sera za kitaifa na kutowa wito kwa serikali kuheshimu njia ambazo wakenya hutumia kujieleza na kuwasilisha lalama zao kama vile maandamano, vyombo vya habari na bunge.

  Ruto awaonya maafisa wakuu wa Jubilee dhidi ya kukigawanya chama

  Naibu wa Rais William Ruto  amewaonya maafisa wakuu wa chama cha jubilee  dhidi ya kutumiwa kuleta mgawnayiko katika chama hicho . Amesema kwamba chama hicho kiliundwa ili kuleta umoja wa wakenya  na maendeleo  na maafisa wake wanafaa kuwa mstari wa mbele kuendeleza ajenda hizo .

  Washukiwa 3 wa Al shabaab wauawa Garissa 

Wapiganaji watatu wa kundi la al shabaab  waliuawa waliposhambulia kambi ya  polisi wa kulinda mipaka ya Yumbis huko garissa .  Polisi wamesema shambulizi hilo la ijumaa usiku lilitibulia kwa haraka na maafisa wa usalama wa kenya .

Jamaa aliyetuma jumbe za matusi kwa mjumbe wa akina mama kushtakiwa Jumatatu

 Mwanamme aliyekamatwa kwa kumtumia jumbe za matusi na vitisho mwakilishi wa akina mama wa tharaka nithi Beatrice Nkatha atafikishwa kortini hapo kesho . maafisa wa polisi walimkamata Joel nyamao siku ya ijumaa na kunasa kadi kadhaa za simu ,simu za mkononi na  chapa za vitambulisho.

 Uchunguzi wa mwili wa mfungwa Simon Gitahi kufanyika Jumatatu

Uchunguzi wa mwili wa mfungwa aliyeaga dunia katika gereza la naivasha utafanywa  hapo kesho  . shirika la IMLU  litaipa familia ya marehemu simon Gitahi mwanapatholojia atakayefanya uchunguzi huo . mfungwa huyo anadaiwa kupigwa na kuteswa na polisi kabla ya kifo chake .

  Mgomo wa wahudumu wa afya Kirinyaga waingia siku ya 26 leo(Jumapili)

Mgomo wa wafanyikazi wa afya huko kirinyaga umeingia siku ya 26 leo  na umeathiri huduma za afya kwa wakaazi . maafisa wa muungao wa wahudumu hao wamesema wanachama wao wataendelea kususia kazi hadi  serikali ya kaunti itekeleze  matakwa yao .

Mtaala mpya wa elimu utaimarisha uchumi-Desai 

 Mtaala mpya wa elimu  katika vyuo vya mafunzo ya kiufundi utasaidia kuboresha uchumi wa taifa .katibu wa kudumu wa elimu ya vyuo vya anuwai Kevit Desai  amesema iwapo mfumo huo utaanza kutekelezwa kuanzia januri ,wanafunzi  watapata ujuzi unaohijika kwa soko la ajira .

   Mkuu wa  Jeshi Ethiopia apigwa risasi 

 Mkuu wa majeshi nchini Ethiopia Seare Mekonnen  amepigwa risasi , waziri mkuu wa taifa hilo Ahmed Abiy amethibitisha kupitia tangazo la runinga mapema leo. Taarifa zinaeleza kwamba kuliwa na jaribio la mapinduzi katika jimbo moja la nchi hiyo   lakini maelezo hayajatolewa baada ya huduma z amtandao kuzimwa .hali ya mkuu huyo wa jeshi pia haijajulikana .

8