radio jambo(1)

Mkusanyiko wa Habari na Matukio Muhimu tarehe 11 Juni 2019

  

Gavana wa Nandi Stephen Sang aachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 1 

Gavana wa Nandi Stephen Sang ameachiliwa kwa  bondi ya shilingi  milioni moja na mdhamini wa kiasi kama hicho au   dhamana ya shilingi laki tano pesa taslimu .Sang amekanusha mashtaka ya uharibifu wa mali ,uchochezi na kutumia vibaya maamlaka yake . Gavana huyo alilala seli  baada ya kukamatwa na maafisa wa DCI huko kapsabet na kupelekwa katika kituo cha Central mjini kisumu .

 

Nitazidi kuwa mkali katika misimamo yangu -Magoha 

WAZIRI  wa elimu George Magoha  amewakosoa wale ambao huchukulia msimamo wake mkali kuhusu masuala kama ujeuri . ameapa kuendelea kuwa thabiti katika maamuzi yake kuhusu masuala  ya elimu .

 Mwanamke ahukumiwa maisha jela kwa kumwua ‘mpango wa kando ‘ wa mumewe

 Mahakama moja huko Naivasha  imemhukumu mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 36 kifungo cha maisha jela  kwa kumwua mwanamke mwingine aliyekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume wake  miaka mitano iliyopita .Cecilia Waruguru Muriithi  alipatikana na hatia ya kumwua   mwanafunzi wa sheria mwenye umri wa miaka 22 juni mwaka wa 2013  baada ya kugundua kwamba alikuwa  na uhusiano wa  kimapenzi na mumewe .

 

Chebukati asema IEBC iko tayari kushughulikia udhaifu wake 

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka  wafula chebukati  anaamini kwamba tume yake itaweza kurekebisha  makosa yalitokea wakti wa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017 . amesema wako tayari kushughulikia changamoto zote za  kimpangilio na kisheria watakazokumbana nazo .

Watoto 3 wa Marehemu Kenneth Matiba wataka kulipwa fidia ya baba yao

Watoto watatu  wa marehemu Kenneth matiba  wanaitaka mahakama kuwapa idhini ya kuitisha malipo  na kusimamia shilingi milioni 504 zilizopewa baba yao . Wanataka kufuatilia malipo ya fidia hiyo na kuhakikisha kwamba usimamizi wa mali yake hauathiriwi . pesa hizo ni fidia ambayo Matiba alipewa na mahakama kwa kukamatwa  na serikali ya KANU alipokuwa akipigania siasa za vyama vingi .

Mwendesha mashtaka mfisadi Kitale apigw afaini ya shilingi 200,000

Mwendesha mmoja wa mashtaka katika afisi ya DPP huko kitale amepigwa faini ya shilingi laki mbili kwa kuitisha na kupokea hongo ya shilingi elfu 60 . amepatwa na kosa la kuitisha rushwa kutoka kwa mlalamishi  ili kukataa ombi la  mshukiwa kupewa dhamana katika kesi ya uhalifu mwaka wa 2014.

Mtoto wa miaka kumi amwua mwenzake Homabay

 Mwanafunzi wa  darasa  la pili katika shule moja ya msingi huko homabay amemwua mwenzake baada ya kumsukuma walipokuwa wakicheza . Watoto hao walikuwa wakicheza hapo jana wakati mmoja alipomzukuma mwenzake ukutani na kumjeruhi .baadaye mtoto huyo alifariki alipokuwa akitibiwa katika  kituo cha afya  cha seka .

  CBK yataka kanuni zake kufuatwa katika kubadilisha noti za kale

 Benki kuu imewaonya maafisa wakuu watendaji wa taasisi za kifedha kuhakikisha kwamba mwongozo wake unatekelezwa kikamilifu kuhusu ubadilishanaji wa noti za zamani za shilingi 1000 ili kuzuia utakatishaji wa fedha . wanaotaka kubadilisha zaidi ya shilingi milioni moja za noti za kale wanahitaji kuwa na idhini maalum kutoka kwa CBK  .

 Mashahidi 33 kuwasilishwa dhidi ya Jackie Maribe na  Joseph Irungu

Upande wa mashtaka umewatayarisha zaidi ya mashahidi 33 katika kesi dhidi ya mwanahabari Jackie maribe na Joseph Irungu   walioshtakiwa kwa mauaji ya mfanyibiashara Monica Kimani  .naibu  mkurugenzi wa  mashtaka ya umma catherine Mwaniki  amesema wanne kati ya mashahidi hao 33 wamelindwa ilhali  watano ni watalaam .kesi hiyo itaanza juni tarehe 25.

 Mmoja afariki huku wanafunzi 2 wakijeruhiwa katika ajali Bungoma

 Mtu mmoja ameaga dunia ilhali wanafunzi wawili wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya barabarani huko bungoma.  Ajali hiyo ilitokea kwenye barabara ya malaba kwenda kanduyi wakati gari dogo walimkuwa wakisafiria kupoteza mwelekeo na kugonga trela .

Kaunti zinafaa kukoma kukopa fedha

Tunahitaji kukomesha mtindo wa kukopa fedha na kuangazia njia mbadala za kutafuta mapato .mtaalam wa ugatuzi Mutakha Kangu  amesema tunahitaji kutumia raslimali za kaunti ili kutafuta mapato zaidi .

 Mwanafunzi wa JKUAT ajeruhiwa na polisi akijaribu kuingia Ikulu

Brian Kibet Bera, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) mwenye umri wa miaka 25 jana alikamatwa na polisi kwa kuingia Ikulu ya Nairobi kinyume cha sheria.
Mwanafunzi huyo, ambaye alikwea lango moja la Ikulu, alipigwa risasi na kuumia katika bega la kushoto na maafisa wa polisi wanaopiga doria kwenye lango hilo baada ya kuchomoa kisu alipoagizwa asimame.
Uchunguzi unaendelea kufafanua nia yake ya kuingia Ikulu kinyume cha sheria na hatua zifaazo zitachukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.

Kenya yafunga mpaka wake na Somalia huko Lamu

Kenya imefunga mipaka yake na Somalia huko Lamu kwa muda usiojulikana huku oparesheni  ya kudumisha usalama ikiendelea . Wakaazi wa vijiji vilivyoko kwenye eneo hilo pia wamepigwa marufuku kufanya bishara  kupitia mpakani

Shule ya Sukwo huko Trans nzoia yafungwa baada ya vyoo kuporomoka

Shule ya msingi ya Sukwo huko Trans Nzoia imefungwa kwa muda baada ya mvua kubwa kusababisha vyoo 16 shuleni humo kuporomoka. Mwenyekiti wa muungano wa walimu na wazazi David Kimam anasema wamefunga shule hiyo kutokana na hofu ya mkurupuko ya maradhi.

Photo Credits: radio jambo

Read More:

Comments

comments