Mkutano watibuka! Wamalwa na wenzake kutoka Magharibi wahofia usalama wao

EZpyJC2XgAIqwdf.jfif
EZpyJC2XgAIqwdf.jfif
Mkutano uliokuwa unaratibiwa kufanywa na baadhi ya viongozi kutoka jamii ya Mulembe ukiongozwa na waziri wa Ugatuzi nchini Eugene Wamalwa, Noah Wekesa, Musikari Kombo na viongozi wengine umeratibiwa kufanyika katika maeneo mengine kwa hofu ya usalama wao.

Viongoiz hao sasa wamelazimika kusubiri kwa kina katika anga tua ya Webuye huku wakitarajia kupata eneo mbadala la kufanyia mkuatano huo.

Katika taarifa nyingine ni kuwa hoteli ya Fairmont imewatumia wafanyakazi wake barua za kutaka kufanyike kwa mazungumzo baada ya kutangaza kuwafuta kazi wiki moja iliyopita.

Taarifa hii inajiri wakati ambapo serikali ilikuwa imeandikia uongozi wa hoteli hiyo barua ya kutaka kuelezea hatua ya kuwafuta wafanyakazi wake kazi.

Umiliki wa Fairmont ulikuwa umesema janga la corona lilikuwa limechangia pakubwa kuporomoka kwa uchumi wake hali iliyopelekea wao kuwatimua wafanyakazi wao.