Mkurugenzi mkuu wa usimamizi wa Mamlaka ya Nairobi Mohammed Badi atakuwa akihudhuria mikutano ya baraza la mawaziri baada ya kula kiapo cha kuweka siri .
Kupitia taarifa iliyotumwa siku ya alhamisi ,Ikulu imesema kwamba rais alishuhudia hafla ya kuapishwa kwa Badi kama inavyohitajika na wote wanaohudhuria mikutano ya baraza la mawaziri au wanaoshughulika na tarataibu za uendeshaji wa serikali .
Msemaji wa Ikulu Kanze Dena amesema kuanzia sasa Mkuu huyo wa NMS atakuwa akihudhuria mikutano ya baraza la mawaziri na kamati zake kwa mujibu wa agizo la rais la tatu la mwaka wa 2020 .
Hafla hiyo iliandaliwa alhamisi kabla ya mkutano wa baraza la mawaziri kufanyika