‘Mlihifadhi pesa ngapi kwa benki?’ shabiki amuuliza DJ Mo na kumjibu kwa ukali

Baada ya sherehe ya siku ya wapendanao illioandaliwa  na msanii  wa injili Size 8 na mumewe DJ Mo na picha kuenea sana katika mtandao wa kijamii ,wakosoaji wao hawakuachwa nyuma bali waliwakosoa na wengi wao kuwa kejeli na hata kuwasifu.

Sherehe hiyo ilikuwa ya kufana na kupigiwa mfano siku hiyo lakini mmoja aliandika swali moja ambalo DJ Mo alimjibu kwa ukali.

" Hapa mlibank pesa ngapi.? shabiki aliyefahamika kama tutormartin aliuliza.

DJ Mo alimjibu na kumwambia kuwa anapaswa kushughulika na mambo yake.

"@ tutormartin kama haukuleta yako wachana na udaku." DJ Mo alimjibu.

Wanandoa hao wawili waliwaeleza wenzao jinsi maisha yao ya ndoa yamekuwa na kuwarai jinsi ya kuishi kwa ndoa.

Awali DJ Mo na Size 8 katika mahojiano walisema kuwa hakuna ndoa iliyokamilifu hata yao yenyewe si kamilifu.

“Mungu ndio siri tumejifunza kukaa pamoja ata nini itokee na kisha kufunga masikio yetu kutoka kwa watu wanaotukujeli na kusema mambo mengi kutuhusu.

Pia tumejifunza kupendana kwa lolote kwa furaha na kwa huzuni, ni ukweli kila mmoja wetu ana udhaifu wake, na ili uweze kushinda udhaifu huo unapswa kukaa.

Na hamna ndoa ambayo ni kamilifu, ina milima na mabonde yake.” Alisimulia DJ Mo.

“Ndoa yetu si kamilifu, na ni ukweli hamna ndoa ambayo ni kamilifu.”Alizungumza.

Wakati huo mkewe alimuunga mkono na kusema,

“Hakuna mtu yeyote ambaye anapaswa kuingia katika ndoa akidhani ni kamilifu,Licha ya hayo ndoa ni kitu cha maana na kizuri sana

Ndoa ni mchakato ambao unafanya kazi maisha na milele.”Aliongea Size 8.