Mlinzi Wa Kanisa Auwawa Huku Kasisi Akinusurika Kifo

mlinzi
mlinzi

Mlinzi mmoja wa kanisa katoliki la Nangina kwa jina Fredrick Ouma aliuwawa na watu wasiojikana usiku wa kuamkia jana.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, watu wanne waliokuwa wamejihami kwa panga walivamia nyumba ya kasisi wa kanisa hilo na kuiba simu pamoja na shilingi elfu tatu kabla ya kasisi huyo kupiga kamsa kuitisha usaidizi.

Akithibitisha kisa hicho kamishona wa kaunti ya Busia bwana Mongo Chimwaga alisema mlinzi huyo aliuwawa kwa kukatwa katwa akiwa katika juhudi za kumsaidia kasisi wa kanisa hilo ambaye alinusurika kifo baada ya kufanikiwa kutoweka.

Aliongezea kuwa juhudi za kuwatia nguvuni washukiwa hao tayari zimeng'oa nanga huku akiwataka wakazi kuwasaidia katika uchunguzi.