Mmiliki wa Shule ya Precious Talent afunguka, asingizia uchochole

unnamed__1569483341_60353
unnamed__1569483341_60353
Huku zoezi la kufanya upasuaji wa miili ya watoto waliofariki baada ya tukio la maporomoko ya madarasa Precious Talent, mmiliki wa shule hiyo Moses Wanaina amefunguka kuhusu tukio hilo.

Moses Wainaina amefuzu na digrii ya kisomo cha biashara baada ya kuhitimu shule ya upili ya Nakuru.

Soma hadithi nyingine:

Moses anasimulia hadithi yake ya maisha ya kichochole hadi kufikia ufanisi wa kumiliki shule hii.

Uwezo hafifu wa kuona na hali ya umaskini wa kutopata karo anasema zilimwandama siku za shuleni.

"Nilianza kujisomesha nikiwa darasa la tatu, matatizo ya kuona vizuri yalinitatiza sana..."

Wainaina amesema kuwa ni ukosefu wa hela uliomfanya kujenga shule iliyokosa mijengo na miundo misingi bora.

Soma hadithi nyingine:

Serikali kupitia ofisi ya DCI inafanya uchunguzi wa tukio hilo na kumkabidhi DPP ripoti hiyo.

Wainaina hana nia ya kujificha au kuikimbia serikali baada ya tukio hilo.

Uwepo wake kila siku katika shule hiyo ni bayana kuwa haogopi lolote.

Takribani wanafunzi 64 walijeruhiwa  katika mkasa huo.

Wanafunzi 60 walitibiwa katika hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta  na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Baadhi ya wanafunzi waliarifu Radio Jambo kwamba waligundua jengo hilo lilikuwa limeinama  na mpindo, mvulana mmoja akamwarifu mwalimu ambaye alimweleza asiwe na hofu na akaambiwa arudi darasani.

Soma hadithi nyingine:

Wazazi waliojawa na hofu walijumuika katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta huku wakisubiri taarifa kuhusu hali za wanao.

Walisimulia kwamba shule hiyo imekuwa ikifinya vyema katika mitihani na gharama yake haikuwa ghali sana ijapokuwa ni shule ya kibinafsi.

Miongoni mwa wanafunzi ni Anthony ambaye alikuwa ameketi kimya darasani  Jumatatu asubuhi  akidurusu huku mwalimu wake akiwa mbele akitayarisha ratiba ya siku. “Niliwasili shuleni saa 6 asubuhi na mwalimu akatueleza tusome  kwa kuwa wanafunzi wote  hawakuwa wamewasili.”
Alisema.