Mmoja aaga dunia baada ya Lori la mafuta kulipuka Busia

31eea187b0bcb719
31eea187b0bcb719
Dereva mmoja ameaga dunia baada ya malori manne ya mafuta kulipuka eneo la Koteko, Teso Kaskazini, walishuhudia ajali hiyo walidokeza kuwa Lori moja la mafuta lilipoteza mwelekeo na kulipuka baada ya kuanguka.

Kikosi cha habari cha gavana wa kaunti ya Busia kilitoa taarifa na kusema baada ya lori hilo kulipuka, mengine matatu yalishika moto.

"Lori la mafuta lilipoteza mwelekeo kabla ya kulipuka na moto huo ukashika malori mengine matatu yaliyokuwa yamebeba mizigo."

Dereva wa lori hilo aliga dunia papo kwa hao huku wengine wakihepa mkasa huo bila majeraha yeyote, nikisaambacho kilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi,8 Agosti.

"Polisi walitoa mwili wa dereva aliyeangamia huku walioshuhudia wakisema wengine walihepa kuepuka moto uliozuka," taarifa ya gavana ilisema.