Mnatarajia mapacha? Msanii wa bendi ya Sauti Sol Polycarp ajibu

Polycarp Otieno almaarufu Fancy Fingers anatarajia kuwa baba hivi karibuni, kupitia kwenye mitandao ya kijamii Polycarp aliposti video na kuandika ujumbe huu ufuatao.
"Wakati wa maajabu kama umesikiza na mtoto akipiga teke katika tumbo la mama yake ni maajabu makuu na wala si madogo, ndugu zangu @SAVARAFRICA AND @IAMCHIMANO mlijawa na mhemko najua lilikuwa jambo tamu sana 

Jambo ambalo ni la maana limekuja na covid-19 ni kuwa nime experience safari hiyo yote kila siku ya wiki, na nashukuru hivi karibuni atakuja."

Mama wa mapacha wawili na mtangazaji Grace Msalame alidokeza kuwa Polycarp na Mandi wanatarajia mapacha.

"IT REALLY IS MIRACULOUS ISN’T IT🤗♥️AND ALSO I’M SEEING TWO👶🏽👶🏽IS THERE SOMETHING YOU’RE NOT TELLING US🤗." Alisema Msalame.

Ni jambo ambalo Polycarp hakukana wala kukubali mbali alisema,

"Vizuri vizuri utafiti umefunguliwa."

Sauti sol inajiandaa kwa kuweka hafla ya tarabu kwa ajili ya kuzindua albamu yao ya 'Night train' itakayo fanyika tarehe 22, Agosti mwaka huu saa tatu usiku.

Huku akiwa kwenye mahojiano Sol alisema kuwa msanii mwenzao anatarajiwa kuwa baba tarehe hizo