Mo Salah aregea katika kikosi cha Misri kitakachopambana na Kenya

Soccer Football - International Friendly - Egypt v Tanzania - "Army Stadium" Borg El Arab, Alexandria, Egypt - June 13, 2019 Egypt's Mohamed Salah during the warm up before the match REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Soccer Football - International Friendly - Egypt v Tanzania - "Army Stadium" Borg El Arab, Alexandria, Egypt - June 13, 2019 Egypt's Mohamed Salah during the warm up before the match REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Kiungo wa Liverpool Mohamed Salah ameregea katika kikosi cha Misri kitakachopambana na Kenya na Comoros katika mechi za kufuzu kwa AFCON mwaka 2021. The Pharaohs wataialika Kenya katika mechi ya ya udunguzi ya kundi G Novemba tarehe 15, kabla ya kukutana na Comoros ugenini siku nne baadae.

Salah ni miongoni mwa wachezaji sita wanaocheza soka ughaibuni waliojumuishwa kwenye kikosi cha Misri.

Hayo yakijiri, rais wa FKF Nick Mwendwa anatarajiwa kufanya kikao na waandishi wa habari leo kuhusiana na hali ya soka humu nchini. Kikao hiki kinajiri wakati ambapo Kenya imeonywa na FIFA kuhusu kushughulikia masuala ya soka kupitia kwa mahakama kuu kinyume na sheria za FIFA. Baadhi ya vilabu vya KPL pia vinataka kusitishwa kwa ligi hio kutokana na matatizo ya pesa yanayoikumba, baada ya mdhamini wake mkuu Sportpesa kutamatisha kandarasi yake.

Nick Mwendwa anadai kua wawaniaji waliokua wakitaka kuwania kiti cha urais wa FKF hawakuchukulia suala hilo kwa uzito. Mwendwa ambaye atashindania wadhfa huo tena kwa muhula wa miaka minne alitajwa kuwa mwaniaji pekee na bodi ya uchaguzi. Mwendwa aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2016 anasema alifuata kanuni zilizowekwa alipojiwasilisha kwa ukaguzi wa bodi hio.

Wing'a wa timu ya raga ya Kenya Sevens Collins Injera anatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika bega lake lililo na jeraha na hivyo hatashiriki mechi za kufuzu kwa Olimpiki ya Africa.

Injera alipata jeraha hilo wakati wa msururu wa Safari Sevens alipochezea Shujaa. Hata hivyo anatarajiwa kupona na kushiriki msururu wa IRB Sevens mwezi Disemba.

Arsenal itakutana na nahodha Granit Xhaka katika siku chache zijazo kujadili kujawa kwake na ghadhabu baada ya kuondolewa uwanjani wakati wa mechi ya jumapili waliyotoka sare ya 2-2 na Crystal Palace. Xhaka anatarajiwa kuregelea mazoezi leo kabla ya mechi ya Arsenal ya kombe la Carabao dhidi ya Liverpool kesho.

FA haitamchukulia Xhaka hatua yoyote baada ya kuonekana akiapa na kuwanyoshea mikono mashabiki wa Arsenal waliokua wakimzomea. Xhaka ambaye amefanya makosa mengi zaidi kuliko mchezaji mwingine katika ligi ya Primia msimu huu, ameondolewa uwanjani katika mechi tatu kati ya tisa za ligi ya Premier alizocheza.

Franck Ribery amepigwa marufuku ya mechi tatu za Serie A baada ya kumsukuma msaidizi wa refa mara tatu katika mechi ya Fiorentina waliyofungwa mabao 2-1 na Lazio jumapili. Kanda za video zilionyesha mchezaji huyo wa miaka 36 akibishana na maafisa wa mechi baada ya kipenga cha mwisho Fiorentina wakipinga bao la ushindi la Lazio kunako dakika ya 89.

Wachezaji wa Fiorentina wanadai Jordan Lukaku wa Lazio alimchezea visivyo Riccardo Sotil kabla ya bao hilo na walikasirika kua refa hakuangalia kisa hicho kwenye kamera za kando ya uwanja, na badala yake kutegemea VAR. Ribery alimsukuma mmoja wa marefa wasaidizi kabla ya kupewa kadi nyekundu.