Mamake Diamond ndiye aliyezua uvumi huo alipomposti kipusa huyo katika instagram na uvumi huo ukakomaa na hata pakatokea habari kwamba huenda wawili hao walikuwa wakipanga kufanya harusi .
Katika mahojiano na Sky Walker ma Creez Favors wa SnS model huyo alijitenga na uvumi huo .
Amesema yeye na Diamond wanajuana kwa sababu wapo katika fani moja na hamna la ziada na wao ni marafiki tu
Pia aliongeza kwamba hana mpango wa kuolewa hivi karibuni .
“It’s very crazy, Napata hata simu kutoka Urusi watu wakiniuliza kwamba mbona sikusema kwamba naolewa na mwanamuziki staa . na sijui mbona kila wakati nikienda kwenye hizi hafla watu wanaweka na mtu mwingine kisha najipata nikitrend’
Alikataa kutoa jibu la moja kwa moja alipoulizw aiwapo anaweza kuzingatiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Diamond .
“ kwa kweli siwezi kusema lolote kuhusu hilo kwa sababu haijawahi kufika kiwango hicho na ikifanyika basi kila mtu atajua kwani sidhani anaweza kutaka uhusiano huo uwe wa siri .ni vigumu sana kwangu kuw ana mtu ambaye yupo machoni pa umma kwa sababu napenda mambo yangu kuwa chini chini lakini huwezi kujua’