Money Trail:Sonko aeleza alikotoa  shilingi Milioni 20  katika akaunti yake .

Sonko
Sonko
Kwa Mukhtasari

  • Sonko amekanusha kujihusiaha na ufisadi
  • EACC ilizifuata pesa hizo hadi katika Akaunti yake
  • Sonko amesema zilikuwa za biashara kabla hajaingia City Hall

Gavana wa Nairobi  Mike Sonko amesema  shilingi milioni 20 zilizopatikana katika akaunti yake na maafisa wa EACC zilikuwa za biashara  alizofanya kabla ya kuwa gavana wa Jiji. Gavana huyo ameshtumiwa kwa kupokea  rushwa ya shilingi milioni 20 kutoka kwa kandarasi yenye kiasi kikubwa cha pesa ya ukusanyaji taka jiji  katika miaka ya kifedha ya 2017-18 ba 2018-2019. Tume ya EACC   imedai kwamba   baadhi ya kampuni zilizoshinda zabuni  hiyo ya shilingi milioni 357 zilihamisha kwa akaunti ya Sonko zaidi ya shilingi milioni 20 .

Sonko  hata hivyo ameyakanusha madai hayo  akisema kamwe hajajihusisha na ufisadi . Pia ameongeza kwamba kaunti ya Nairobi imelipa kodi  zote  isopokuwa kiasi kilichorithiwa kutoka kwa uatawala wa gavana wa zamani Evans Kidero .Sonko  amesema kaunti ya Nairobi imelipa zaidi ya shilingi bilioni tano kama ushuru .

Pia kaunti ya jiji haijatoa shilingi milioni 5o  zinazofaa kuwalipa wafanyikazi wa jiji mishahara yao ya mwezi  huu. Gavana  huyo  alihojiwa siku ya jumanne kwa zaidi ya saa nane  katika makao makuu  ya EACC na kurekodi zaidi ya taarifa 13 tofauti .