Moses Kuria

Moses Kuria apuuzilia mbali ripoti ya BBI, adai ni ‘feki’

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amepuuzilia mbali ripoti ya BBI iliyozinduliwa juma lililopita huku akidai kuwa ni ‘ghushi.’

Kupitia ujumbe kwenye mtandao wake wa Twitter, Kuria ambaye alikuwa akimjibu wakili Donald Kipkorir alisema,” Imejikita kwenye mfumo wa uongozi kupitia bunge, waziri mkuu na wakuu 12 wa kanda. BBI halisi sio bonoko iliyozinduliwa juma lililopita katika ukumbi wa Bomas.”

Kipkorir alikuwa amedai kuwa anatazamia mapendekezo ya BBI yaidhinishwe kuwa sheria.

Mugabe Aliacha Pesa Taslimu Shilingi Bilioni 1, Gazeti Ya Herald Yatoa Ripoti

Aidha alisema kuwa Rais Uhuru Kenyatta atahitajika kubuni kamati ya wataalamu ili kuunda mswada utakaopeleke kufanyia katiba marekebisho.

Kisha, Uhuru na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga watazunguka kote nchini wakinadi sera za miswada hiyo na “kusaka zaidi ya saini milioni 9 kutoka kwa wananchi.”

Kipkorir aidha aliendelea kusema kuwa saini na miswada hiyo itawasilishwa kwa tume ya IEBC na baadaye kwa mabunge ya kaunti.

Siku Chache Baada Ya Kutuzwa, Mkewe Mbusii Asherehekea Siku Ya Kuzaliwa

“Jumla ya kaunti 40 badala ya 24 wakiidhinisha mswada huo basi utaelekezwa kwa bunge la kitaifa na utahitaji kupitishwa na idadi ya wabunge walio wengi. Kisha Uhuru ataidhinisha kuwa sheria,” alisema.

Kuria juma lililopita alishtumu wana ODM kwa kutaka BBI kuidhinishwa kupitia kura ya maamuzi.

Aidha alisema kwamba mchakato huo wa kura ya maamuzi hautagharimu taifa kitita kikubwa sana cha fedha.

Alisema kuwa shilingi bilioni 7 zinafaa kutumiwa kuimarisha kiwanda cha kahawa, bilioni 4 kulipa wakulima wa sukari na nyingine bilioni 4 kuanzisha kiwanda cha viazi, shilingi bilioni 4 kununua mchele kutoka Mwea na Ahero na nyingine bilioni 4 kuwasaidia wakulima wa miraa.

Sarakasi: Jinsi Mgonjwa Alivyotoroka Kutoka Hospitali Baada Ya Upasuaji

 

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO.

 

Photo Credits: The Star

Read More:

Comments

comments