Moses Kuria apigia debe safari ya Miguna Miguna kurejea nchini

Moses-Kuria-Uhuru-Park
Moses-Kuria-Uhuru-Park
Mbunge wa Gatundu  Kusini Moses Kuria amedai kuwa wakili Miguna Miguna anafaa kuruhusiwa kuingia na kuwa huru nchini Kenya.

Tamko la Moses linajiri siku chache baada ya wakili huyu mwenye utata Miguna Miguna kuweka wazi kuwa atasafiri Kenya mapema mwaka ujao.

Katika mitandao ya kijamii, wakili huyu ambaye ana uraia tata alisema kuwa haogopi kusafiri nchini tarehe 11, Januari 2020.

Kulingana na mbunge huyu, Miguna alikuwa mkenya alipokuwa akihudumu katika ofisi ya kinara wa ODM Raila Odinga.

Kuria anahoji kuwa swala hilo lilikamilika baada ya kuidhinishwa kwa katiba ya 2010.

Moses ameongeza kuwa ni vyema Miguna apewe pasipoti yake .

"Nilimwandikia aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo Raila Odinga nikimjulisha kulikuwa na raia wa Canada aliyekuwa akifanya kazi katika afisi yake kwa jina Miguna Miguna," alisema Kuria .

"Kupitia aliyekuwa waziri wa uhamiaji Gerald Otieno Kajwang', Raila alisema Miguna alikuwa Mkenya na hata kutoa pasipoti yake aliyokuwa amepokezwa Kisumu," Kuria aliongeza katika chapisho mtandao wa Facebook.