Moses Kuria ataka wabunge kuangalia timu ya mawaziri ya Matiang'i

Mbunge wa Gatundu South Moses Kuria amependekeza ya malezi ya kamati ya wanachama 27 katika bunge kusimamia baraza la mawaziri wanao ongozwa na waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i.

Moses ameandikia spika Justin Muturi akisema kuwa kamati hiyo itawaunga mkono utambuzi wa halhamashauri kuu. Pia anataka kamati hiyo kuitwa (Parliamentary Development Coordination Committee).

Rais Uhuru Kenyataa mwezi jana aliweza kumteua waziri Matiang'i kuwa msimamizi wa (National Implementation and Communication Cabinet Committee).

Baraza la mawaziri linalojumuisha makatibu wote wa mawaziri, mwanasheria mkuu Paul Kihara na mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kinyua.

"Kutoka kwa yaliyotangulia,ni muhimu bunge kuwa na jukumu lake kwa msaada wa halhamashauri kuu na utambuzi wa agenda nne kuu," Alisema katika barua yake.

Matiang'i amewakilishwa na katibu wa hazina wa baraza la waziri Henry Rotich. Timu yake itahakikisha kuwa kuna uratibu wa mawasiliano na maendeleo ya mipango ya serikali na miradi.

Kamati pia inaweza kupendekeza kusitishwa kwa baadhi ya mikataba na kupendekeza hatua za kisheria.

Wakiripoti katika kamati ya Matiang'i ni timu ya kiufundi ikiwahusisha makatibu wakuu 14, inapaswa kujulikana kama utekelezaji wa maendeleo ya kitaifa na kamati ya kiufundi yaani (National Development  Implementation Technicak committee).

Kulikuwa na maneni kuwa uteuzi wa Matiang'i kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya baraza la mawaziri ilifanyika ili kupunguza ushawishi katika serikali wa naibu rais William Ruto.

Ruto amekuwa mwangalifu katika miradi ya chama cha jubilee.

Pia wizara zinaweza kusimamiwa na kamati husika katika nyumba, Kuria alisema kuwa nafasi ya mapendekezo kuwa kuratibu matarajio ya sheria na bajeti.

Moses kuria aliweza kuandika majina ya viongozi watakao kuwa katika kamati hiyo.

Miongini mwa walioratibiwa na Kuria ni; kiongozi wa wengi Aden Duale, kiongozi wa wachache John Mbadi, Benjamin Washiala, Junet Mohamed, Jimmy  Angweny, Rebert Mbui, Cecily Mbarire, Chris Wamalwa, Sabina Chege, Kathuri Murungi, Timothy Wanyonyi, Esther Passaris, Fatuma Gedi, Bashir Abdhulahi, Rachel Nyamai, Kareke Mbiuki, Mishi Mboko, Danson Mwahoko, Soipan Tuya, Caleb Kositany, Florence Bore, Beatrice Adagala,  Dan Wanyama,Rosa Buyu, Opiyo Wandayi na Ngunjiri Wambugu.