Moses Wetangula apoteza kiti chake kwenye chama cha Ford Kenya

Chama cha Forum for the Restoration of Democracy Kenya (FORD Kenya), kimempiga makasi Seneta wa Bungoma Moses Wetang'ula kutoka kwa wadhifa wa kiongozi wa chama hicho.

Chama hicho kimemteua Mbunge wa Kanduyi, Wafula Wamunyinyi kama kaimu kiongozi wa chama hicho.

Uamuzi huo wa kumvua Wetangula kutoka kwa wadhifa huo ulifikiwa Jumapili, Mei 31, wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Kitaifa la chama hicho.

https://twitter.com/Phelixi/status/1267017920858685441

Wetangula alikashifiwa kwa kushindwa kuwa kielelezo cha amani katika chama hicho, kushindwa kuongoza chama hicho kutwaa ushindi kwenye uchaguzi na kutatiza uteuzi wa mwaniaji katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2017.

NEC pia ilimlaumu seneta huyo kwa udhaifu kwenye uongozi wake kwa chama hicho na pia kutotoa motisha, ubadhirifu wa fedha kutokana na kutajwa kila mara katika sakata ya KSh250 milioni ya dhahabu feki ya Dubai mwaka 2019.