Chidzuga Mwangoka ( sio jina lake halisi ) aliacha kazi yake Novmba mwaka jana baada ya kumafnyia bosi wake kwa zaidi ya miaka 10 kwa ajili ya malipo duni, kazi nyingi na muda mrefu wa kufanya kazi .
Hata hivyo baada ya mwezi mmoja, bosi wake ambaye ana biashara ya utengezaji wa vitambaa vya nguo alimpigia simu na kumtaka arejee kumfanyia kazi kwa ahadi ya kuteeleza kila alichokitaka.
“ Nilikubali kurejea kumfanyia kazi," amesema Mwangoka.
Lakini Mwangoka anasema bosi wake alianza kumtaka amfanyie vitu vya kushangaza kama vile kumkanda . “ Mwanzoni, nilifikiri maombi yake haya hayakuwa na hila kwa sababu angelalama kuhusu maumivu ya misuli na uchovu’ Mwangoka amesimulia .
Alianza kumkanda bosi miguu, mikono na mgongo.
“ Hata hivyo alianza kunitaka nimkande mapajani na nikaanza kupata ugumu kidogo’ Bosi naye akawa mkarimu na hata akampa zawadi ya Friji na runinga ya inchi 42. “ Nilifikiri kuacha kazi kulimfanya agundue kwamba alihitaji msaidizi katika jumba lake kubwa alimoishi na mkewe wa tatu’.
Mfanyibiashara huyo anayeishi katika mtaa wa kifahari wa kizingo ana watoto wanne aliowapata katika ndoa zake mbili za hapo awali. Wake zake wawili wa zamani walifariki na wanawe wanne wanaishi Uingereza .
Mwanamume huyo hana mtoto na mkewe wa tatu. Kuelekea mwezi Disemba mwaka jana alianza kutoa maombi ya kustaajabisha hasa wakati wa msimu wa sherehe. Mwangoka anasema bosi wake alianza kumtaka amkande mwili mzima.
“kilichonishangaza ni kwamba angeniita katika chumba cha kumkanda na ningempata akiwa uchi wa mnyama amelala kifudifudi akinitaka nimkande," amesema Mwangoka.
Hatua yake ya kulalamika ilivutia vitisho vya kufutwa kazi. Alikubali kumkanda na hata katika sehemu zake siri . Kulingana na Mwangoka bosi wake alikuwa akimtaka alitumie bomba la maji pamoja na sabuni ya mwarubaini ili kumsafisha mkondo wa kwenda haja kubwa .
“ Baada ya hapo angekwenda chooni kuendesha kabla ya kurejea na kutaka nimkande tena’ amesema Mwangoka
“ Baada ya hapo jamaa alikuwa akirusha mashuzi makali yenye harufu ya kumwangamiza hata mende. Nilihofia angeniambukiza ugonjwa usiojulikana".
Alitumia fursa ya ukarimu wake kuitisha mkopo wa shilingi 8000 alizotumia kununua simu za kisasa ili kuweza kuchukua picha za vitendo hivyo kama ushahidi. Afisa kutoka shirika la Muhuri Francis Auma anasema kisa hicho ni tukio halisi la dhulma za kimapenzi.
Tukio lenyewe limeripotiwa katika kituo cha polisi cha Central chini ya nambari OB 33/21/01/2020. Auma amesema visa vya dhulma za kimapenzi Mombasa vimeongezeka hasa katika mitaa ya Kizingo, Nyali na Tudor.
“ Maeneo haya ya kifaharai yana usiri mkubwa. Polisi hawapigi doria katika mitaa hii kwa sababu ni ya watu mashuhuri na wenye uwezo mombasa ambao wanazingatia sana usiri na mambo yao", alisema Auma .
Amewahimiza polisi kukichunguza kisa kilichomfika Mwangoka na kumkamata bosi wake .