‘Mpango wa kando’ alipoamua kujileta kwa sponsor baada ya kuachwa hoi kwa miezi mitatu

Mwanamke   aliyekuwa amewekwa kama mpango wa ando aliamua kujichukulia  hatua mikononi mwake baada ya kwenda kwa sponsor wake na kupiga kambo huko akidai kwamba jamaa alikuwa amemtelekeza kwa miezi mitatu tangu kuanza kwa janga la corona .

Watu waliovutiwa na tukio hilo katika eneo la Bahati ,Nakuru walishangaa ujasiri wa mwanamke huyo kwa sababu inafahamika kwamba mwanamke wa pembenei anafaa kujiweka kama siri lakini kwa sababu jamaa ambaye ana mke na watoto alimkodishia nyumba na kumuacha huko kwa  muda huo wote bila mawasiliano ,mpango wa kando aliamua kwenda kwake kubisha mlango na kumueleza mke  wa sponsor wake kuhusu masaibu yake .

Wengi walionekana kutamaushwa na hilo kwa sababu wakati mwingi makabiliano makali huzuka kati ya mke wa mtu na mpango  wa kando lakini licha ya kufahamu hatari hiyo ,mwanamke huyo aliamua kuhatarisha usalama wake ili kwenda kumkabili sponsor akiwa kwake . Wakati mke wa ponsor aliposikia yote aliyosema yule mpango wa kando ,alishindwa  cha kufanya na kama mwenyeji mzuri alimkaribisha ndani yule mpango wa ando ,kumpa chai na kumuita mumewe akimueleza kwamba mgeni wake alikuwa amekuja .

‘ Watoto wangu walikuwa wanalala,singeanza kupigna na huyo mwanamke na isitoshe nilijua kwamba mume wangu alikuwa na mwanamke wa pembeni’ amesema mwanamke huyo

Alijichukulia nguo zake na kuanza kufua hapo nje huku mume wake na mpango wa kando wakiendelea kulumbani ndani ya nyumba .Mwanamke huyo alikuwa akilalamika mbona sponsor wake hakuwa akizipokea simu zake au kumtumia pesa za kununua chakula au kulipa kodi ya nyumba .Jamaa alisikika akijitetea kwamba hajakuwa akienda kazini muda wote huo na hakuwa na fedha za kumtumia mpango wa kando .  Alimrai mpango wa kando akome kupza sauti juu huku akimtaka waondoke ili kuzungumzia mambo yao mbali na nyumbani kwake lakini yule mpango wa kando hakutaka hilo ,alitaka jamaa ampe pesa na  apokee simu zake kwa sababu kulingana naye ,yeye sasa alikuwa mke wa pili na hakutaka kujua iwapo yule jamaa  ana mke  tayari .

Mama mwenye nyumba hakusema jambo na mumewe baadaye alijaribu kumuomba msamaha akieleza kwamba hakuwa  na nia ya kumuoa mwanamke yule mpango wa kando lakini maji tayari yalikuwa yamezidi unga na  usaliti wake yaonekana angeulipia baadaye . Mkusayiko wa watu nje ya nyumba yao bila ulizidisha aibu na sarakasi nzima hiyo ilidumu kwa  zaidi ya siku nzima huku mpango wa  akitoka ,tena akarejea akisema yuataka kusuluhishwa kwa  utata ule na pia kutunzwa kama mke .