Mpende msipende,niko hapa! Maraga asema hatang'atuka hadi muda wake ukamilike

Jaji mkuu nchini David Maraga amesema hatang'atuka mamlakani hivi sasa hadi pale hatamu yake ya kuhudumu itakapokamilika.

Akizungumza alipokuwa anazindua mpango wa dijitali wa kusajili kesi mbalimbali mahakamani, Maraga amesema hatatoka kamwe katika wadhifa wake kwani kuna mengi ambayo yanahitajik kufanywa.

"I noticed when the president of LSK spoke it was like he was bidding me goodbye but I am still here," he "When a judge goes on retirement, he or she gets a letter to go on leave from the chief Registrar of Judiciary and that I think will be in November." maraga

Chini ya mfumo huo mpya, mawakili, polisi, DPP na wananchi kwa ujumla wanatarajiwa kujisajili kupitia mfumo huo ili kuwa ndani ya data za mahakama.

Maraga amesema mfumo huo utapunguza siku za kusikilizwa kwa kesi na hata wakati wa kuandikisha kesi mahakamani na hivyo kuwasaidia wananchi walioko nchini na kimataifa.