Mpenzi Wa DK Kwenye Beat amuenzi siku yake ya kuzaliwa

Mwanamziki wa nyimbo za injili DK Kwenye beat anasherehekea siku yake ya kuzaliwa. Mchumba wake Shanice Wangeci amemuenzi kwenye mtandao wa Instagram akimshukuru kwa kuwa mtu ambaye anamsikiliza wakati wote.
"Heri ya siku ya kuzaliwa mpenzi wangu. Asante sana kwa kuwa rafiki yangu, mwendani wangu na kunisikiliza ninapotaka mtu wa kunisikiliza. Asante kwa kunipa sababu za kuangaza. Wewe ni kila kitu na ninatumai siku hii ni mojawapo wa siku nzuri maishani mwako."

DK atamba mitandaoni miezi kadhaa iliyoisha baada ya kuhusika kwenye mahusiano ya ngono na mwanafunzi wa chuo kikuu.

Baadaye mpenzi wake, Shanice, alifuta picha zote katika mtandao wake wa Intagram lakini kwa sasa hivi amerudi na inaonekana kwamba mapenzi ya wawili hawa yanazidi kutamba.