Mpenzi wangu alimpenda babangu mzazi! Ole wenu mnaopendana na slayqueens

Kuwa muangalifu kuhusu  mtu unayemuahidi ndoa .Kuna watu ambao wanaingia katika maisha yako wakiwa na  nia tofauti na watu wengi watakupa  visa vya jinsi walivyokuwa waathiriwa .

Lakini kuna uchungu  ambao hauwezi kutulizwa kwa mtu kusema pole . Uchungu  wa aina hiyo ni kama anaopitia  Jared . Baada ya uhusiano wa kimapenzi uliodumu kwa miaka mitatu na hatima yake ikaonekana kuwa ndoa ,Jared hakuwa na shaka kwamba mke wake atakuwa  Stacy . Iwapo ungemuambia kwamba miaka miwili ijayo hawangekua pamoja basi papo hapo angekuita adui mkubwa wa maendeleo yake . Unaweza kufikiri  kwamba unamjua mtu hadi wakati anapofanya jambo fulani kisha unagundua kwamba my friend  humjui kabisa .

 Can You imagine   baada ya  Jared kumtambulisha   Stacy kwa wazazi wake ,ghafla  mpenzi wake alianza kubadilika tabia na kufanya vitu ambavyo havikueleweka . Pindi Stacy alianza kupata shughuli ambazo hazikuwa katika mipango .mawasiliano  kati yao pia yalianza kukatika na  maneno matamu yaliokuwa ya kawaida kama vile  I miss you  na I love you yalianza kuwa nadra sana kutoka  katika kinywa chake . Jared aligundua kuna tatizo  na kweli hisia zake hazikumsaliti . Yamkini ilikuwa bayana kwamba Stacy alikuwa  keshatekwa fikra na mtu  mwingine lakini  Jared alishangaa mbona basi asiseme wazi ili waachane rasmi . Kumbe makubwa yalikuwa njiani yamemgonja Jared ! Stacy alikuwa kapendana na babake Jared. Msichana  bila aibu aliamka siku moja na kumuambia Jared kwamba ‘ You are not mature enough for me,but your dad is’ .

 

Kwake Jared ,yote haya yalikuwa kama ndoto lakini kwa kweli ndio ulikuwa mwanzo wa ngoma . Hakuelewa ni vipi msichana ambaye wamekuwa naye katika uhusiano  kwa muda huo  mrefu anavyoweza kusema kwamba yuamtaka babake ambaye wakati huo alikuwa na  umri wa miaka 65.Baba mzazi hakuwa amesema lolote na Jared alipata ugumu sana kumkabili babake ili kumshtumu kuwa katika uhusiano na mchumbake. Hilo halingekuwa tu kumkosea heshima  mzee wake lakini pia ni ufichuzi ambao ungemkwaza mamake Jared . Bila kujua ,babake Jared alikuwa  hii mbegu ya  ‘wazee vijana’ .Wamekomaa kiumri lakini vitendo vyao ni vya kitoto .Starehe kwake hazikumtosha na ilikuwa siri iliyofahamika na wengi kwamba Baba Jared alikuwa mpenda sketi sana .Alikuwa hapitwi na mwanamke lakini hakuna aliyejua kwamba angevuka mipaka hadi kushiriki  uhusiano wa kipamenzi na mchumba wa mtoto wake .

Usaliti huo  mara dufu wa babake na mpenzi wake ulimpa uchungu sana asijue atafanya nini hadi alipopata ujasiri wa kumkabili babake ili kumuuliza . Mzee  alipopewa  madai hayo alisema –‘ Mwanangu ,mwanamke huyo anakushinda na niligundua hilo pindi ulipomleta hapa mara ya kwanza .Alichukua nambari yangu na tangia hapo tumekuwa tukiwasiliana.I don’t think  she’s the right woman for you’. Baba alisema bila hata kuwa na haya .

Ufichuzi huo kutoka kwa babake ulikuwa ithibati ambayo Jared alihitaji kuipata ili kukubali kabisa kwamba ni kweli   Stacy alikuwa ameshaamua kuacha uhusiano wao na kufanya uhusiano mwingine na babake .  aibu gani kwa mzee wa hadhi kama yake kufanya kitendo kama kile ! Jared alijutia mbona aliwahi kukutana na Stacy na akagundua  mapenzi yalimfunika macho kwa sababu tabia zake zilikuwa sio za mtu muamiminifu ambaye angemfanya kuwa mke wake siku za baadaye lakini sasa kila taswira ilikuwa imeachwa wazi peupe .

Ungefanya ni iwapo ungejipata katika nafasi ya Jared?