Mpenziwe Tecra Muigai Omar Lali akamatwa kuhusiana na kifo chake

Polisi huko Lamu wamemkamata mwanamme  anayedaiwa kuwa mpenzi wa marehemu Tecra Muigai  aliyeaga dunia baada ya ajali kutokea katika nyumba waliokuwemo .

Lali Omar alikamatwa  baada ya kubadilisha taarifa yake mara kadhaa kuhusu  hali iliyopelekea kuaga dunia kwa Tecra .Inadaiwa wawili hao walikutana mapema mwaka huu  katika Hoteli ya Peponi wakati Tecra aliposhindwa kulipa bili ya hoteli yake. Lali anadaiwa kuwa Beach boy ambaye ni changudoa wa kuwapunja fedha wanawake na aliitumia fursa hiyo  kumsaidia Tecra ili kuepuka kuifedhehesha familia yake .

Baadaye binti huyo wa mmiliki wa Keroche Breweries alimpenda Lali  na mara kadhaa walisafiri hadi Lamu kwa raha zao katika hoteli mbalimbali .

Polisi wanaendelea na uchunguzi wao ili kufahamu kilichosababisha kifo cha Tecra .