bhang

Mpishi akiri kutumia bangi ‘kuongeza ladha mpya’ kwenye chakula

Mpishi mmoja alitiwa mbaroni baada ya kukiri kutumia bangi kama kiungo cha kuongeza “ladha mpya” kwenye mapishi yake.
Mpishi maarufu sana nchini Italia amekamatwa na polisi kwa ulanguzi wa dawa za  kulevya baada ya kupatikana na mimea ya bangi.
Carmelo Chiaramonte mwenye umri wa miaka 50, ni mpishi mtajika sana katika eneo la Trecastagni nchini Italia. 
 Yeye  hushiriki katika kipindi cha mpishi bora kwenye televisheni.
Chiaramonte aliwaambia polisi kwamba alikuwa akijaribu mapishi mapya na alitaka kutumia mimea hiyo ya bangi kama “”viungo  vya kuongeza ladha katika mapishi yake.”
Alipokamatwa na maafisa wa polisi kwake,
Chiaramonte hakuonyesha wasiwasi wowote.
Aliwakabili polisi kwa ukweli kwamba hangenuia kuiuza mimea hiyo bali alitaka kutumia kuleta “ladha mpya” kwenye mapishi yake.
Alijitetea kwa polisi kwamba yeye ni  “mshauri wa vyakula vya kiasili katika upishi wa kisasa Mediterenia.”  gazeti moja la Italia limeripoti.
Hata hivyo, polisi walipofanya msako zaidi walipata mimea   nyingine ya bangi  katika gari lake.
Mpishi huyo alitiwa mbaroni na anatarajia kesi yake kuwasilishwa  kwa tuhuma za ulanguzi wa dawa za kulevya.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments