Msamiati wa Siku na Yusuf Juma, tarehe 22 Septemba 2014

Ni asubuhi na unatandika kitanda chako baada ya kuamka. Kwanza unatandaza mashuka mawili juu ya godoro na unafuatilia kwa kuzifunika na mfarishi kisha unamaliza shughuli hiyo kwa kuweka mto katika upande wa kitanda unayotumia kupumzisha kichwa chako. Neno "mfarishi" ndio msamiati wa siku ya leo na katika lugha ya kimombo, mfarishi hujulikana kama "duvet".