Msanii Amani anavyotofautiana na mmewe

Mtindo upo nchini wa wasanii wa nyimbo za kidunia kubadilika ghafla na kuanza kuimba nyimbo za injili na kuokoka.

Wasanii kama Size 8, Kush Tracey, Lady B, Collo, Wahu ni katika ya wasanii ambao walibadilika na kuimba nyimbo za injili.

Msanii Amani hajaachwa nyuma katika mchakato huu na hii leo alikuwa katika Bustani la Massawe kipindi kinachoruka kupitia masafa ya Redio Jambo akizungumzia kuhusu jinsi anavyoona maisha yake yamebadilika pindi tu alipoanza kuimba nyimbo za kumtukuza mungu.

Soma mengine hapa:

 Huku akionekana kumficha bwanake katika mahojiano hayo, Amani alidokeza jinsi walivyokutana.

“Tulikutana kabla niokoke. Nilimwambia mimi nataka kuokoka, nikamuuliza wewe utaokoka akasema hayuko ready halafu nikamueleza kuwa itabidi tumebreak up kama hataokoka.”

Amani anasema kuwa anapenda sana kuweka anayoyafanya tofauti na bwanake ambaye huwa hafichi lolote kuhusu uhusiano wao. Msanii huyu amedokeza kuwa alitamani kuolewa na kujaliwa watoto kama marafiki zake. Kutoka aokoke, msanii huyu amefanya vibao kama Upendo, My God  kati ya nyingineo.

Amani ameweza kufanya kazi na Teddy B na Mainswitch katika nyimbo zake mpya.

Soma hapa: