Msanii chipukizi Acey tayari kupambana na magwiji nchini

Acey
Acey
Msanii Grace Vivian Were, almaarufu, Acey ni chipukizi ambaye amejihami ili kupambana na wasanii ambao tayari wamevuma nchini.

Jinsi miaka inasonga, umaarufu wake Acey umekuwa ukitamba huku nyimbo zake ziki pokelewa vyema na mashabiki na watangazaji nchi nzima.

Huku akianza kazi ya usanii mwaka wa 2015, tayari amefanikiwa kurekodi nyimbo mbili, 'Nimekutoka' na 'Sugar' na uvumi wake tayari umeanza kusambaa.

Lakini je alianza aje?

"Nilianza usanii mwaka wa 2015 baada ya kuchochwa na marafiki zangu kuwa nina sauti ya kutoa nyoka pangoni." Alisema Acey.

Nakumbuka msanii Pascal Tokodi alianzisha shindano la usanii ambapo aliwataka wasanii kuiimba wimbo wake 'Sitaki' huku mshindi akijishindia kitita cha elfu hamsini na nafasi ya kurekodi naye.

Basi marafiki zangu walinishauri nijaribu, na niliibuka mshindi." Alisimulia Acey ambaye ni mzaliwa wa Vihiga.

Baada ya ushindi ule, hapo ndipo aliamua kuufanya mziki kwa kina na pia kama kazi inayompa riziki.

Ni kipi kilimpa hamsisho ya kurekodi 'Nimekutoka?

Hii ngoma ina siasa. Nili rekodi mwaka wa 2017 baada ya kuvunjwa moyo na mpenzi wangu. Jamaa alinivunja moyo na nikabidi nimtoke.

Ngoma zangu huwa true story ama zina relate na marafiki zangu na pia mimi ndio najiandikia ngoma zangu. 

Acey aliongeza kuwa wimbo wa 'Sugar' ni wimbo wa mapenzi kwani ilimbidi autunge baada ya marafiki zake kuteta kuwa amekuwa akiimba nyimbo za huzuni.

Ujumbe wake kwa mashabiki.

Hii ni job kama ile ingine tunaichukulia seriously pia. Watu wasituchukulie kama tumepotea kwani kwa mfano pia mimi nimeenda shule lakini nimechagua kufanya muziki.

Ningeambia wakenya wa support Kenyan music kwani hatuwezi enda mbali kama hatupati support hapa nyumbani.