Msanii Eric Omondi asimulia alivyopatana na Churchill

Mvunja mbavu mkenya Eric Omondi ameyakumbuka maisha yake ya mwanzoni kabla ya kujiunga na kipindi cha Churchill.

Eric Omondi aliwashangaza wengi baada ya kurejea kwenye show hio baada ya kupotea kwa miaka saba. Siku ya Alhamisi, Churchili ilifanyika mjini Naivasha na siku hiyo Eric Omondi alikuwa mtaani huo.

"Mwaka 2006, nikiwa mwaka wa pili katika chuo kikuu cha Day star, Nilikuwa mkuu wa sherehe (mc) fulani ambayo churchili alihudhuria," Eric alisema.

"Alifurahishwa na uwezo wangu. Nilikuwa nataka kumuomba nambari yake ya simu na kabla sijamuomba yeye aliniomba yangu. Nilingoja miaka miwili kabla ya kupokea simu yake mwaka 2008. Aliniuliza kama nipo tayari kufanya shoo."

 

Eric pia alieleza jinsi alivyofunzwa kupiga shoo na Churchil. "Nilikuwa nafanya kazi ya kuongoza sherehe tofauti tofauti na watu walinieleza baadaye kuwa niliwafurahisha kila wakati. Siku moja nilifahamu kuwa churchili atahudhuria sherehe furani hapo shule jambo lililo nifurahisha sana," Eric alisema.

"Sikutaka kuongoza shoo yenyewe ila nilipewa nafasi hio siku hio. Nilikariri shairi pamoja na kuipa hadhira hadithi zilizowaacha wakiumwa na mbavu zao huku churchill mwenyewe alibaki tu kaduwaa usiku mzima," Eric alisema huku mashabiki wakimshangilia.

Baada ya shoo ,Churchill alimkujia Eric na baada ya miaka miwili alimpigia simu kumwalika kupiga shoo na huo ndio uliokuwa mwanzo wake Eric.