Msanii Kambua azungumza kuhusu safari ya kujifungua kwa upasuaji

kambua
kambua
Msanii wa nyimbo za injili na mrembo kupindukia, Kambua alijifungua kifungua mimba wake mwaka huu kupitia upasuaji, al maarufu Caesarian section, kwa kimombo.

Kambua alifunguka hivi majuzi na kusema kuwa bado anaendelea kupata nafuu akisema kuwa kovu hiyo itachukua mda kupona.

Alisema,

“This is me thanking God that I can fit into one of my pre-preggers dresses. My body has changed alot and I am embracing it all. I stretched in ways I never knew were possible! Isn’t God amazing? And then went through a CS (story for another day). Recovering from it is not a joke!” she wrote on Instagram.

Alisema kuwa kwa sasa kazi kuu ni kujichunga na kumlea mwanawe kwa namna bora huku akisema kuwa licha ya mwili wake kubadilika kwa kiwango kikuu, anamshukuru mola kwa kumfanya mzazi na hajutii lolote.

“I have chosen to be kind to myself. Giving myself the time I need to heal, and also to nurture my toto. I haven’t even told you about the edges I’ve lost because of breastfeeding! But I have no regrets. It’s all been worthwhile. Next year I will think about diets and workouts. (That baby pouch will need to go). But for now I’m counting my blessings, enjoying the chubby cheeks and snug clothes lol.”

Kambua hakusahau kuzungumzia watu ambao tabia zao ni kuwatusi na kuwaaibisha wenzao kwa misingi ya miili yao na maumbile.

Aliwashauri wazazi kutojali sana kuhusu miili yao baada ya kujifungua huku akiwakumbusha kuwa itawachukua mda kabla miili yao iregeleekama zamani.

“Please be kind to your friends postpartum. There’s so much pressure to “snap back”, without considering that being alive after birthing a child is a miracle in itself. Watu wa, “umenona”, please have several seats over there...”