benga

Msanii wa benga ya kikuyu azungumza baada ya kupata ajali

Msanii maarufu wa kikuyu Kamande wa Kioi amewataka wakenya wazidi kuomba kuhusu ajali ambazo zimezidi kuongezeka humu nchini Kenya.

Hii ni baada ya msanii huyo kuhusika katika ajali barabarani siku ya alhamisi usiku akielekea nyumbani kwake. Gari lake liligongana na basi ya Nazigi sacco kwenye barabara ya kamiti.

Watu wawili waponea kifo baada ya lori kuwaka moto

Akizungumza na gazeti la The Star kupitia njia ya simu, msanii huyo alithibitisha kuwa ametolewa hospitalini. Kamande alipata majeraha madogo na alikimbizwa katika hospitali ya Nairobi women.

Tukio hili linajiri mwezi mmoja tu baada ya msanii maarufu wa kikuyu John De Mathew kupoteza maisha yake katika ajali. De Mathew alifariki mnamo agosti 18, baada ya gari lake kugongana na lori huko Thika eneo la Blue Post.

Kamande alionyesha picha la gari lake lililogongwa katika mitandao ya kijamii, huku akimshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yake. Kamande amewataka madereva wa matatu kuwa waangalifu zaidi.

Vile vile alihimiza taifa mzima haswa wapenzi wa benga kote nchini, kuweka wasanii wao kwenye maombi.

 

Wakenya wamuomba Dennis Itumbi ampachike Maribe mimba!

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments