Msemaji wa serikali Cyrus Oguna aeleza jinsi alipigania maisha yake kutokana na corona

Wiki chache baada ya msemaji wa serikali Cyrus Oguna kupatikana na maambukizi ya corona na kisha kulazwa hospitali kwa matibabu hatimaye ameeleza jiinsi alipigana na virusi hivyo alipokuwa hospitali.

Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii, Oguna alisema kwamba wakati ambao alilazwa alikuwa na uchungu mwingi kwenye kifua chake ambao ulisababisha awe na shida ya kupumua.

Oguna alisema kuwa alipigana na shida ya kupumua usiku mzima hadi pale madaktari walikuja kesho yake kuanzisha matibabu yake.

https://twitter.com/SpokespersonGoK/status/1306846850557804545

"Kwa ugumu mkubwa singefanya chochoye yaani singepumua uchunguzi wa X-ray ulifanywa lakini mita chache kuenda kwa x-ray ilikuwa ndoto mbaya sana

ata nikiwa kwenye oksijeni ilikuwa ngumu kupumua hata kusonga ilikuwa uchungu sana si kwa kifua tu mbali kila sehemu ya mwili ilikuwa uchungu

vitu vidogo kama kugeuka kitandani halikuwa jambo rahisi hamu ya chakula niliokuwa nimebaki nayo iliisha kabisa." Oguna Aliandika.

Baada ya siku chache Oguna hakuonyesha mabadiliko yeyote katika hali yake ya afya ambapo iliwabidi madaktari kupandisha spidi ya oksejeni yake.

"Sikufahamu kitu chochote kwenye wadi yangu hata kazi ya madaktari waliokuwa wanafanya, kila mmoja akija na kunipa dawa tofauti

nakuangalia kilichokuwa kinatendeka kwenye mashine yangu Akilini mwangu nilijua tu mambo hayako sawa lakini nilijiambia kuwa napaswa kuwa na nguvu."

Wakati huo msemaji huyo alisema kuwa alikuwa anasikia sauti kwenye akili yake zilizomshangaza kama alikuwa hai ama amefariki.

Kulingana naye hakuwa anazungumza sana hata kumaliza sentensi moja.