Mshangao! Fahamu jinsi wanaume walivyobadilishana wapenzi Busia

wife_exchange_2_696x522__1568112421_49414
wife_exchange_2_696x522__1568112421_49414
Wanaume wawili Busia wamewashangaza walimwengu baada ya tukio la kubadilishana mabibi baada ya ubuyu kuzuka hali ya kutoaminiana.

Kabla ya tukio hilo, Lilian Weta alikuwa bibi wake Kelvin Barasa.

Barasa alimleta mwanamke mpya na kumtambulisha kwa Lilian. Mwanamke huyu mpya alikuwa ameolewa na Christopher Abwire.

Soma hapa hadithi nyingine:

 Katika mahojiano na kituo cha utangazaji hapa nchini, Lilian alisimulia:

"Alirudi nyumbani na kunieleza kwamba amekuja na cousin wake kutoka Mombasa. Nilipomuuliza atarudi lini akanikasirikia. Ghafla nikaona mwanamke amevaa jacket ya mme wangu."

"Akanipa taarifa kwamba kuanzia sasa kuendelea yeye ni bibi mpya na kwamba niondoke au anidunge kisu."

Kelvin Barasa alijitetea kwamba alipatana na Millicent na akampenda

Soma hapa hadithi nyingine:

"Tulipatana kwa barabara na nikamwambia maneno matamu na akakubali. Sijali anachofanya mke wangu na wala simuhitaji tena. Tulibadilishana."

Kelvin alimwambia mkewe Lilian aende akaolewe na bwana wa Millicent. Taarifa hizi zilipelekea Lilian kumpigia simu kaka yake.

"Nikasimulia kakangu kitu na ambacho Kelvin alisema na kakangu aniambia nifanye hivyo."

Mmewe Millicent, Chrisopher alisema kuwa yuko freshi kumuoa Lilian.

Soma hapa hadithi nyingine:

"Alifunguka kuwa amefukuzwa na mmewe. Bibi yangu alikuwa ashaniacha kwa hivyo tukaamua tuwaache hao wadanganyifu."

"Kutoka nimuoe Lilian, maisha yangu yamebadilika. Sina mawazo. Nakula kwa wakati unaofaa..."

Lilian ana watoto 4 ilhali Millicent ana watoto 2.