Mshoneshe vitenge! Dennis Itumbi afichua siku atakayofunga ndoa

Imekuwa mda sasa tangia wakenya waanze kujiuliza ni siku gani ambayo bwana Dennis Itumbi atafunga ndoa ili warembo waweze kutulia.

Kwa sababu zinazojulikana, wengi walikuwa na ushawishi mkuu kuwa angefunga ndoa na mwanahabari Jacque Maribe, ila alvunja mioyo ya wengi alipofichua kuwa wawili hao ni marafiki tu na hakuna hisia za mapenzi baina yao.

Katika mahojiano ya moja kwa moja, Itumbi alisema,

‘THE BIBLE SAYS A GOOD WIFE IS A GOOD GIFT FROM GOD AND MINE IS STILL BEING WRAPPED BY GOD.

MY ARMS ARE OPEN SO WHEN HE IS DONE HE WILL DROP IT AND IT WILL FALL INTO MY HANDS.’

Aliongeza,

‘I WILL ANNOUNCE THE WEDDING LATER, MAYBE THE NEXT FEBRUARY 29TH AFTER THIS YEAR.

YOU WILL ALL BE INVITED EITHER AS A MEMBER OF THE CONGREGATION, A PASTOR OR AS A BRIDE.’

Alipoulizwa je mbona yeye hutumia alama ya reli ya#OneManOneWoman kila anapochapisha ujumbe wowote katika mtandao wake wa Instagram, Itumbi alisema kuwa yeye anaamini uhusiano wa mwanamme mmoja na mwanamke mmoja.

Haya basi, hatuna budi ila kungoja kwa udi na uvumba harusi yake na cha muhimu kumjua atayemchagua kama mke wake na atakayefaidika na shairi zake.