D8SaFQ2XoAAKtiU.jfif

Mshukiwa katika kuteketezwa kwa jumba la Malik Heights Kujisalimisha

Mshukiwa mkuu katika kisa cha kuteketezwa kwa Jumba la Malik Heights jijini Nairobi ambapo mali ya thamani yakiwemo magari ya kifahari 69 iliteketea anatarajiwa kujisalisha kwa polisi leo.

D8SaFQ2XoAAKtiU.jfif

 

Aliambia wandani wake kwamba atajisalimisha baada ya kupata habari kwamba alikuwa akisakwa na polisi kuhusiana na kuteketea kwa jumba hilo siku ya Jumatatu wiki hii.

 

Soma pia Kaza mkanda, hali ngumu kiuchumi yaja, bajeti ya kitaifa yapunguzwa

Mshukiwa alinaswa katika kamera za CCTV ndani ya Jumba hilo lililoko katika barabara ya Ngong akiwa na mtungi ambao polisi wanashuku ulikuwa na mafuta.

 

moto.jfif

 

Kisha anaonekana akiyamwaga mafuta hayo kwa magari yaliokuwa yameegeshwa na kisha moto kuzuka.

Alionekana akitoroka mbio baada ya moto kuanza.

Soma pia: PATANISHO: Kijana wangu atoe mbuzi au anipe elfu kumi

jumba.jfif

Soma pia: Rihanna ndiye mwana muziki tajiri wa kike Duniani

Inasemekana mshukiwa wakati mmoja alihudumu kama wakala wa kampuni moja ya kuuza magari iliyopoteza magari yenye takriban thamani ya shilingi nusu bilioni.

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments